Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amewaonya wafanyabiashara wilayani humo na kuwaagiza kuacha kurejea na kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi wakati serikali imewatengea maeneo yanayofaa kwa ajili ya biashara,kwani kufanya hivyo ni kukwamisha juhudi za usafi wa miji.
Onyo hilo amelitoa katika kikao maalum na wadau mkoani humo kwa ajili ya maandalizi ya kuuwasha mwenge wa uhuru ambao kitaifa utawasha Aprili 2 mwaka huu mkoani hapa katika uwanja wa sabasaba mjini Njombe
Amesema pamoja na kuwa wapo katika maandalizi ya kuuwasha mwenge lakini maendeleo ya mji wa Njombe bado ni suala muhimu.
Amesema wafanyabiashara wote wametengewa maeneo yao rasmi kulingana na aina ya biashara wanazofanya lakini wamekuwa wakikiuka utaratibu uliowekwa.
"Tulishawawekea maeneo yaliyo rasmi na wapo wapo wanatekeleza ila kuna baadhi wanakaidi jambo ambalo siyo zuri" alisema Kissa.
Ameongeza kusema kuwa serikali haiwezi kufumbia macho suala hilo kwakuwa nia yake siyo tu kuuweka mji katika hali ya usafi na mpangilio mzuri bali wafanyabiashara wauze bidhaa zao katika mazingira mazuri na ya usafi.
Alibainisha kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya ameelekeza kila baada ya wiki mbili usafi ufanyike katika maeneo mbalimbali ya mji wa Njombe.
Mkurugenzi wa Njombe mji Kurthum Sadick alisema mkoa wa Njombe unatarajia kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ili kushuhudia uwashwaji wa mwenge hivyo jambo muhimu kwa wananchi ni kuwakarimu wageni hao.
Amesema suala la ukarimu biashara na huduma mbalimbali ni muhimu kwani kutawavutia wageni kuja kuwekeza mkoani hapa.
"Limeongelewa suala la ukarimu ni kweli tuna kazi kubwa sote tuwe mabalozi maana nimewahi kwenda dukani ukifika mfanyabiashara anakuangalia tu" alisema Kurthum.
Wananchi walioshiriki katika kikao hicho walisema ujio wa mwenge mkoani Njombe utatoa fursa za kiuchumi na utekelezaji wa miradi mingine ambayo itaibuliwa na mwenge.
Walisema watashirukiana katika kutoa elimu ili mapokezi ya wageni yapewe heshima inayostahili katika mkoa wa Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...