

Mkutano ukiendelea
Baadhi ya wajumbe wa Timu ya Kitaifa ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala wakionesha vitendea kazi walivyokabidhiwa baada ya kuzinduliwa kwa timu hiyo katika tukio lililofanyika Wizara ya Fedha na Mipango katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru akipokea kwa niaba ya Serikali Hundi Kifani ya shilingi milioni 460.4 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Bw. Peter Malika, zitakazoiwezesha Timu ya Kitaifa iliyoundwa kwa ajili ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala (Alternative Project Financing – APF National Facilitation Team) kutekeleza majukumu yake kikamilifu.PICHA ZOTE NA MICHUZIJR-MMG





Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe, Lawrence Mafuru wakijadiliana jambo na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Charles Mwamwaja kabla ya Uzinduzi wa timu ya Taifa ya Uwezeshaji wa mkakati wa ugharamiaji wa miradi ya maendeleo kwa njia mbadala uliofanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibara Mhe.Aboud Hassan Mwinyi akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe, Lawrence Mafuru kabla ya Uzinduzi wa timu ya Taifa ya Uwezeshaji wa mkakati wa ugharamiaji wa miradi ya maendeleo kwa njia mbadala unaofanyika leo jijini Dodoma,kulia ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Charles Mwamwaja,





Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru (aliyekaa katikati) kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Aboud Hassan Mwinyi na kushoto kwake ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamaja, wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Kitaifa ya Kuwezesha Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kutumia njia mbadala (Alternative Project Financing – APF National Facilitation Team), baada ya kuzinduliwa kwa Timu hiyo katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.PICHA ZOTE NA MICHUZIJR-MMG
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...