UBALOZI wa Tanzania nchini Ukraine umetoa tamko kuhusiana na hali ya sintofahamu ya kiusalama inayoendelea nchini humo.
Taarifa iliyotole wa na Ubalozi wa Tanzania nchini humo, imeshauri kuwa wote wanaodhani kukaa Ukraine kwa sasa sio salama waondoke nchini humo.
Aidha kwa wazazi wenye watoto wanaosoma nchini humo na wanataka watoto wao warejee kwa muda hadi hapo uvumi wa kutokea vita utakapoisha, wafanye utaratibu binafsi wa kuwarudisha watoto wao nyumbani kwa kutumia ndege za abiria zinazofanya safari kutokea Ukraine.
Pia ubalozi umeshauri wanafunzi wanaotaka kurudi nyumbani wawasiliane na uongozi wa vyuo wanavyosoma na kukubalina kuendelea kwa masomo kwa njia ya mtandao (Online) kipindi chote watakachokuwa nje ya Ukraine.
Home
HABARI
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UKRAINE WATOA TAMKO, WANAODHANI KUKAA NCHINI HUMO SIO SALAMA WAONDOKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...