Na.Khadija Seif Michuzi TV
KUELEKEA siku ya wanawake duniani Chama cha Wanawake Wafanyabiashara nchini (TWCC) kinaandaa maonesho ya bidhaa na utoaji tuzo kwa wajasiriamali wa viwanda na biashara.
Maonesho hayo yatafanyika Machi 3 hadi 8 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Moja, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa chama cha Wanawake Wafanyabiashara nchini (TWCC) Mwajuma Hamza amesema utoaji tuzo utafanyika Machi 9 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
“Lengo la Maonyesho haya na tuzo ni kuhamasisha wajasiriamali kuongeza nguvu katika kazi zao, pia kukuza uchumi wa taifa kupitia kazi wanazozifanya."
Pia, Mwajuma amesema utoaji tuzo hizo ni kusherekea Mafanikio wanayoyapata Wanawake katika Sekta ya viwanda na biashara.
“Tuzo hizi zilizunduliwa rasmi Januari 29 mwaka huu kupitia mkutano wa mwezi wa wajasiriamali ulifanyika hapa Jijini Dar es Salaam."
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara nchini (TWCC) Mercy Sila amesema Tuzo hizo zinalenga kuonesha Mchango wa Mwanamke Mjasiriamali katika kukuza uchumi wa nchi na Maendeleo ya jamii.
Sila ameongeza kuwa Wanawake ni nguzo muhimu katika Maendeleo ya jamii yoyote, pia wanaweza kufanya Mapinduzi makubwa katika Sekta ya Viwanda na Biashara.
“Naishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha Mazingira ya Biashara nchini ambapo wanawake wengi wameanzisha Biashara na Viwanda vidogo ambavyo vimeongeza kipato, kuzalisha ajira pamoja kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi."
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la TradeMark East Afrca (TMEA), Monica Hangi ameeleza kuwa wametenga shilingi bilioni nne kufanikisha Mradi huo wa kujengea uwezo wanawake wa Tanzania kufanya biashara.
“TMEA inafanya kazi na wadau mbalimbali katika kukuza biashara kikanda na kimataifa, tulimua kudhamini tuzo hizi na itandelea kuwa mdhamini mkuu kutokana na lengo kubwa ni kuhakikisha biashara za wanawake zinakuwa na kuleta tija kwa taifa."
Mkurugenzi wa Trademark Afrika Mashariki (TMEA) Monica Hangi akifafanua zaidi kuwa Shirika hilo limetenga bilioni 4 kufanikisha Mradi wa kuwajengea uwezo Wanawake nchini kufanya Biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara nchini (TWCC) Mwajuma Hamza akieleza namna Tuzo zitakazofanyika Machi 9 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city zenye lengo la kuwainua Wanawake Wajasiriliamali zilizoandaliwa na chama hicho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...