VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kutumia nafasi zao kuwahamasisha wananchi wanaochukua mikopo kwenye mabenki na taasisi za fedha kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuweza kurejesha mikopo hiyo na kujijengea uaminifu wa kukopesheka.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Meneja wa Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu (BoT) ,Victoria Msina wakati wa kufunga semina ya waandishi wa habari wa fedha na uchumi iliyofanyika jijini Mbeya.

Msina amesema kuwa kukopa kwa malengo na kurejesha mikopo Kwa wakati kunatoa nafasi ya kukopesheka na hivyo kupata mikopo zaidi na Kwa riba nafuu.

" Hii itawasaidia wao katika shughuli zao za kiuchumi, kuweka vizuri mizania ya mikopo ya benki na taasisi husika na kufanya ziweze kukopesha watu wengi zaidi, nyinyi kama wanahabari ambao mnapata uwelewa wa masuala ya fedha mnaweza kuwa daraja imara la kutoa elimu hii Kwa wananchi," alisema Bi Msina.

Aidha, amesema kuwa wananchi wengi hawazingatii elimu ya utunzaji mzuri wa noti zetu ili zidumu kwa muda mrefu zaidi na kupunguza gharama kwa serikali kuchapisha fedha zingine.

"Pia kuna suala hili la utunzaji wa noti zetu, bado kuna watu wanakunjakunja hovyo noti au kuzishika wakiwa na unyevunyevu, hali ambayo inapunguza kwa kiasi kikubwa uhai wa fedha hizo na kulazimisha serikali kuingia gharama za kutengeneza zingine, kupitia elimu ambayo mmepata nyie waandishi mtakuwa mabalozi wetu kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza fedha katika hali nzuri, " amesema Msina.

Pia amesema wananchi wanapaswa kujihusisha na shughuli za ujenzi wa taifa na kutangaza kazi mbalimbali za ubunifu.

"Nyie waandishi mkawe wasemaji wao hawa wananchi ambao wanafanya kazi zinazochangia maendeleo ya taifa pamoja na fursa mbalimbali ambazo, ama zimeendelezwa kidogo, au hazijaendelezwa kabisa ili kuvutia wawekezaji kuziendeleza na kwa jinsi hiyo kuchangia maendeleo ya taifa, aliongeza kusema Bi Msina.

Pia alitaka mtandao uliojengwa Kati ya maafisa wa benki kuu na waandishi wa habari utumike kwa ajili ya kukuza habari za biashara, uchimi na fedha Kwa kushirikiana uzoefu mbalimbali.

Semina hiyo ya siku tano iliwahusisha waandishi wa habari wa masuala ya fedha na uchumi kutoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Rukwa Songwe na Katavi na ilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo na uwelewa wanahabari hao kuhusu  masuala ya kifedha na uchumi.




Kaimu Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki , Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Vicky Msina akizungumza leo wakati akifunga semina ya mafunzo ya siku tano iliyoandaliwa na BoT kwa waandishi wa habari za Uchumi Biashara na Fedha, kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Dar es Salaam na Zanzibar na kufanyika kwenye ofisi za Tawi la Benki Kuu Mbeya.

Afisa Uhusiano Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Lwaga Mwambande akizungumza kabla ya kufungwa rasmi kwa semina ya mafunzo ya siku tano iliyoandaliwa na BoT kwa waandishi wa habari za Uchumi Biashara na Fedha, kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Dar es Salaam na Zanzibar na kufanyika kwenye ofisi za Tawi la Benki Kuu Mbeya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...