Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa nchi wanachama wa Bonde la Mto Nile kuepuka migogoro, ambayo inasababishwa na umiliki wa rasilimali za pamoja baina ya nchi zinazounda umoja huo.

Dkt. Mpango ameyasema hayo katika maadhimisho ya miaka 16 tangu kuanzishwa umoja wa Bonde la Mto Nile, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, amesema nchi wanachama wanapaswa kufurahia mafanikio yaliyopatikana kutokana na mshikamano katika miaka yote tangu kuanzishwa kwake.

Dkt. Mpango amesema Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ya (Mto Nile: Urithi Wetu kwa Amani na Ustawi) inawakumbusha nchi wanachama kuhamasisha amani na maendeleo katika jamii za nchi husika na ustawi wa watu katika bara la Afrika.

“Ni dhahiri kuwa kila nchi ina mipango yake ya maendeleo kwa ajili ya Wananchi wake, hata hivyo pale inapotokea tuna rasilimali za pamoja, hatuna budi kushirikiana na kukubaliana namna bora ya kufaidika na rasilimali hizo bila kusababisha migogoro”, amesema Dkt. Mpango.

“Tuna jukumu la kukumbushana kuwa sisi ni wa moja, na tunao wajibu wa kuhakikisha tunailinda na kuitekeleza ajenda yetu ya umoja wa Afrika, ajenda inayoeleza ‘Afrika Tuitakayo’ ambayo ina lenga nchi zetu kuwa na amani, ustawi na usalama kwa raia wote”, ameeleza

Kwa upande wake, Waziri wa Maji nchini, Mhe. Jumaa Aweso amesema Serikali ya Tanzania ipo bega kwa bega na nchi wanachama wa Umoja wa Bonde la Mto Nile katika kushirikiana masuala mbalimbali ya maendeleo ya umoja huo. Hata hivyo, Mhe. Aweso ameshauri umoja huo kuongeza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano katika shughuli za umoja huo sanjari na lugha za Kifaransa na Kiingereza.

“Asilimia 10 (10%) ya Waafrika wanategemea Bonde la Mto Nile, naamini kuimarika umoja wetu, tutaimarisha bara zima la Afrika na hata dunia kwa ujumla. Njia pekee ya kuimarika umoja huu, ni umoja na mshikamano wetu”, amesema Mhe. Aweso.

Neye, Mkurugenzi Mtendaji wa Sekretarieti ya Bonde la Mto Nile, Mhandisi Sylvester Matemu ameipongeza Serikali ya Tanzania kuandaa na kufanikisha mkutano huo ikiwa ni mara ya pili kuandaa tangu mwaka 2017.

Nchi wanachama wa Bonde la Mto Nile ni Tanzania, Uganda, Sudan, Rwanda, Kenya, Ethiopia, Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na Sudan Kusini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wadau kutoka nchini mbalimbali wa Bonde la Mto Nile, katika maadhimisho ya miaka 16 tangu kuanzishwa umoja huo.
Baadhi ya wadau wa umoja wa Bonde la Mto Nile wakishiriki maadhimisho ya 16 tangu kuanzishwa kwa umoja wa Bonde hilo, maadhimisho hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akitembelea Mabanda ya Maonesho yaliyoandaliwa katika maadhimisho hayo ya miaka 16 tangu kuanzishwa Bonde la Mto Nile.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...