Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
JITIHADA za serikali za kusimamia utekelezaji wa kanuni ndogo ya vifurushi, promosheni na ofa maalum imeboresha ushindani na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye ghamara ndogo za simu na intaneti.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jabiri Bakari alisema hayo wakati wa mkutano wake na Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF).
Alisema kutokana na jitihada hizo imeboresha ushindani kupitia kuweka kikomo cha vifurushi sokoni, RTD kwa vifurushi visivyo na mwisho wa matumizi ili kuwezesha wateja wanaopendelea kuvitumia pamoja na kuidhinisha na kufuatilia bei za huduma za mawasiliano ya simu zinazotolewa na watoa huduma ili kumlinda mteja.
Pia kuhakikisha kuwa wateja wanalipia huduma kama inavyostahili kuendana na gharama za uzalishaji.
Alisema utafiti mbalimbali duniani unaonyesha kuwa, gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini Tanzania, zipo chini tofauti na nchi nyingine duniani.
Vile vile gharama za kawaida bila kujiunga na kifurushi, pamoja na gharama zilizounganishwa na kifurushi nazo zimeshuka.
Alisema utafiti huo unaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya sita kwa Afrika kwa kutoza bei ndogo, alitaja pia utafiti mwingine unaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya 21 kati ya 155 duniani kwa kutoza bei ndogo.
" Utafiti wa kimataifa unafanywa dunia uzima. Ukienda kwenye huo utafiti unaonyesha na kushabiana kinachofanyika Tanzania
" Huo ni utafiti tofauti, gharama zake zinategemea na gharama za uwekezaji katika eneo husika," alisema.
Pia alisema Tanzania inaongoza kwa kuwa 'bundle' rahisi na salama Afrika na duniani kwa kila 'settings'
Alisema bei ya mwingiliano kati ya watoa huduma imeshuka kutoka sh 2.6 kwa dakika mwaka 2021 hadi Tzs 2.0 kwa dakika mwaka 2022 hali hiyo imesaidia kushusa gharama za kupiga simu kwenye mitandao kiasi kwamba hivi sasa tofauti ya kupiga simu (gharama kwa dakika) ndani ya mtandao mmoja na kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine ni ndogo sana hivyo kuwaondolea wateja adha ya kuwa na simu zaidi ya moja ili kuepuka gharama.
Alisema Machi 21 mwaka 2012 idadi ya lain za simu zimeongezeka kutoka 51,210,914 hadi 55,396,190 Januari mwaka huu.
Pia idadi za laini za simu zinazotumia huduma za pesa mtandao zimeongezeka. kutoka 27,326,938 Machi 21 hadi 32,720,180 Januari 2022
Naye Mkurugenzi Masuala ya Sekta TCRA, Dk Emmanuel Manasseh akizungumzia kifurushi katika simualisema kumekuwa kukisemwa kuwavifurushi hivyo vinaisha kwa haraka lakini Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya majaribio mbalimbali ili kuhakikisha watoa huduma Santos kile walichoahidi kwa watumishi.
Alitaja vitu vinavyosababisha kumaliza 'bundle' kwa haraka kuwa ni kuongezeka kwa kasi ya mtandao kwenye simu janja mfano kutoka 3G hadi 4G.
Pia alisema ubora wa video na picha unavyoongezeka maana yake matumizi nayo yanaongezeka" Tuna application mbalimbali kwenye whatsap zinafanyiwa update mara kwa mara unazo zinatumia data.
" Watumiaji wengi wa simu Kuna vitu vinaendelea kwenye simu yake lakini mtumiaji hajui. Uwepo wa application nyingi, nyingine hazitumii hivyo zinamaliza bundle,'alisema.
Pia alisema TCRA imeelekeza watoa huduma kutengeneza application ambayo watumiaji wanaweza kufuatilia matumizi yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka hiyo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Emmanuel Manase akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari ,jijini Dar es Salaam.
Mhariri wa Uhuru Jane Mihanji akichangia wakati wa Mkutano wa Wahariri na TCRA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahariri na watumishi wa TCRA katika mkutano wa kuangalia mafanikio ya utoaji huduma za Data wakati Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk.Jabiri Bakari akijibu hoja mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...