Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wanafunzi wanaosoma shule mbali mbali za sekondari katika wilaya ya Njombe,wamepewa taulo za kike (Pedi) ili kuwanusuru na ukosefu wa vipindi vya masomo darasani kwa kuto kwenda shuleni pindi wanapoingia kwenye siku zao za hedhi.

Taulo hizo zimetolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe Mh,Neema Mgaya kwa shule tano mpaka sasa tangu mpango huo ulipoanza mwaka 2020 mpaka sasa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi taulo kwa wanafunzi 280 wa shule ya sekondari Mpechi na shule ya Sekondari Mabatini,Mbunge huyo amesema mpango huo ni endelevu kwake ikiwa lengo kubwa ni kuwasaidia wanafunzi wakiwemo wanaoishi katika mazingira magumu.

“Ndani ya wilaya ya Njombe kuanzia mwaka 2020 nilipoanza mpango wa kuwasaidia watoto wa kike, tumeshafikia shule tano na katika shule hizo tumefikia wanafunzi 1480 ukijumlisha watoto 280 tuliowafikia siku ya leo”alisema Neema Mgaya

Ameongeza kuwa “Hili ni hitaji muhimu kwa watoto wetu,kwasababu ili mtoto aweze kukaa ndani ya darasa na kumsikiliza mwalimu akiwa kwenye zile siku zetu ni lazima awe salama lakini watoto wengi wanashindwa kuja shule kwasababu ya kukosa kifaa hicho kinachomuwezesha kukaa kwa usalama”

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amemshukuru mbunge huyo kwa msaada kwa kuwa unasaidia kupandisha viwango vya taaluma katika wilaya hiyo.

“Umeweza kuwafikia wananfunzi zaidi ya 1408 kwa kweli ni msaada mkubwa sana ambao utaweza kuinua kiwango cha taaluma katika wilaya yetu ya Njombe kwa kuwa zile siku ambazo mtoto atashindwa kufika shule atakosa kitu kikubwa sana”aliseama Kissa Kasongwa.

Margareth Masoli ni mkuu wa shule ya sekondari Mabatini amesema kundi la watoto waliopata msaada huo ni kubwa sana hivyo anaamini msaada huo utawafanya watoto kuwa huru.

“Tunashukuru sana kwa zawadi hizi ambazo umewaletea watoto na tunataraji watoto watakuwa huru kwasababu wanapokuwa huru ndipo wanapofanya vizuri kitaaluma”alisema Masoli

Diana Nyigu ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Mabatini na Ester Mgombela ni mwanafunzi wa kidato cha nne wameshukuru kwa msaada huo utakaowawezesha kufanya vizuri katika masomo yao huku pia wakimshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa madarasa yaliyotokana na fedha za uviko kwa kuwa yamesaidia kupunguza uwingi wa wanafunzi kukaa katika darasa moja.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe Neema Mgaya akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi watano watakao tumia kwa Muda wa mwaka mzima wakiwa kwenye siku zao katika shule ya sekondari Mabatini halmashauri ya mji wa Njombe.
Waanafunzi wa shule ya sekondari Mpechi halmashauri ya mji wa Njombe wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kupokea taulo za kike kwa mbunge wao.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mpechi wakifurahia pamoja na mbunge baada ya kupata msaada wa taulo za kike kutoka kwa mbunge wao.
Mbunge Neema Mgaya akizungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Mabatini alipotembelea katika shule hiyo.

Mbunge Neema mgaya akigawa Pedi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Mpechi.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...