MIRADI YA UMWAGILIAJI NAMTUMBO HAINA TIJA KWA WANANCHI.
NA Yeremias Ngerangera…Namtumbo
Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA)kimedai miradi ya umwagiliaji iliyopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma haina tija kwa wakulima kwa kuwa haizalishi kama ilivyotarajiwa na kuwaneemesha wakulima katika maeneo yaliyojenga miradi hiyo.
Mratibu wa ufuatiliaji wa rasilimali za umma kutoka MVIWATA katika sekta ya kilimo wilayani Namtumbo Shifla Ally katika taarifa yake alisema wilaya ya Namtumbo inamiradi 14 ya umwagiliaji na katika miradi hiyo ni kiwango kidogo kinachofanyiwa kazi hali inayofanya kutoonesha tija kwa wakulima tofauti na malengo ya serikali.
Shifla Ally alidai walifuatilia miradi ya umwagiliaji katika kata ya kitanda,Limamu na kata ya Ligera ambapo pamoja na changamoto zingine walibaini kutokuwepo na usimamizi unaotokana na walengwa wa mradi kutoona faida ya miradi hiyo kwa kuwa hawakushirikishwa toka awali na kuitazama miradi kama sio yao.
Jovinari Mhagama aliyekuwa mwenyekiti wa skimu ya umwagiliaji ya Njomlole alisema kuwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo hapakuwa na uwazi,uwajibikaji ,ushiriki na ushirikishwaji kwa wakulima na viongozi wa serikali katika kupanga na kutekeleza mradi huo ndio maana wananchi au wakulima hawaoni umaana wa miradi hiyo kwa kutowashirikisha toka awali ili waione miradi hiyo ni ya kwao.
Ofisa umwagiliaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Eleuter Mndendemi alisema kuwa kati ya miradi 14 ya umwagiliaji katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo hakuna mradi wowote uliokamilika bali wakulima wachache ndio wanaonufaika na wengine wamekosa kutokana na kutokamilika kwa miundombinu hiyo ya umwagiliaji.
Mnung’a Shaibu Mnung’a mkurugenzi wa millennium art group alitoa mwongozo wa utekelezaji wa miradi ya serikali mambo yanayopaswa kuzingatia ili miradi hiyo iweze kuwa endelevu na kuwa na tija katika jamii.
Alitaja swala la uwazi,uwajibikaji,ushirikishwaji katika utekelezaji wa miradi utawafanya wananchi kufuatilia na kushirikishana katika ngazi mbalimbali za maendeleo ya miradi yao ili waweze kuilinda na kuiendeleza baada ya mradi kukamilika .
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Dkt Julius Kenneth Ningu pamoja na mambo mengine aliwataka wakulima kujikita katika kilimo cha mazao mchanganyiko ili kujipatia kipato na changamoto zilizojitokeza katika skimu za umwagiliaji zitafanyiwa kazi alisema mkuu wa wilaya huyo.
MVIWATA inatekeleza mradi wa utawala bora na ufuatiliaji wa rasilimali za umma katika wilaya ya Namtumbo likiwa na lengo la kuimarisha mamlaka za serikali za mitaa ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuongeza uwazi ,uwajibikaji,ushirikishwaji kwa wananchi ili miradi inayotekelezwa iweze kuleta tija kwa wananchi .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...