Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mamia
ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walijitokeza katika viwanja vya
Mlimani City mwishoni mwa wiki kuchukua namba zao za kushiriki mbio
maarufu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2022.
Waandaaji wa mbio hizo walisema muitikio ulikuwa mkubwa kwani washiriki wengi walifika kwa muda na kufanya zoezi liende vizuri.
Wengi
waliochukua namba ni washiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager km
42 na Tigo km 21 half marathon huku pia wa km 5 wakijitokeza na wengine
wakiendelea kujisajili.
“Usajili kwa ajili ya mbio za km 42 na 21 tayari umefungwa lakini bado tunauza namba za Km 5, walisema waandaaji.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi alisema zoezi hilo
lilienda vizuri kwani washiriki walipata namba bila kusubiri muda
mrefu.
“Zoezi
lilikuwa limepangiliwa vizuri kwani tumeshuhudia washiriki wakiingia na
kuondoka kwa haraka,” alisema huku akitoa wito kwa wakazi wa Arusha
wajitokeze kwa wingi kwa ugawaji wa namba utakaoanza Jumanne.
Zoezi
hilo litafanyika katika Hoteli ya Kibo Palace Jumanne Februari 22, 2022
na Jumatano Februari 23, 2022 kuanzia saa nane kamili hadi saa moja kwa
siku hizo mbili.
Zoezi
hilo litamalizikia Moshi ambapo namba hizo zitatolewa katika viwanja
vya Chuo Kikuu Cha Ushirika Alhamisi Februari 24, 2022 kuanzia saa sita
mchana hadi saa kumi na mbili jioni, Ijumaa Februari 25, 2022 kuanzia
saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni na Jumamosi February 26,
2022 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
“Washiriki
waliojisajili wanatakiwa kuzingatia muda wa zoezi hili katika vituo
husika ili kuepusha usumbufu na zoezi likishafungwa hakutakuwa na
ugawaji wa namba siku ya mashindano,” walisema waandaaji hao.
Waliongeza
kuwa usajili kwa ajili ya mbio za kilomita 5 bado unaendelea kwa njia
ya Tigo Pesa kwa kubonyeza *149*20# na kwamba usajili pia utafanyika
katika vituo vya kutolea namba.
Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).
Wadhamini
wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC
Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water. Wasambazaji rasmi ni
GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles na
Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).
Katika
hatua nyingine, Kwa mujibu wa waandaaji wa Kilimanjaro Marathon, kwa
mara ya kwanza kutakuweko na maonesho yanayojulikana kama Kili Expo (The
People's Expo) ambapo wadhamini na wadau wengine wa mbio hizo watapata
fursa ya siku tatu za kuonyesha bidhaa na huduma wanazotoa, maonyesho
ambayo yanatarajiwa kufanyika kati ya Februari 24-26, 2022, katika
viwanja vya MoCU.
"Maonyesho
haya pia linakusudiwa kuwapa umma uzoefu wa muda mrefu wa mbio za Kili
Marathon; pia kwa mwaka huu wanaotarajia kushiriki mbio hizo watapata
fursa ya kuchukua namba zao za ushiriki eneo la chuo kikuu cha Ushirika
badala ya eneo la hotel kama ilivyokuwa miaka ya nyuma”, ilisema taarifa
hiyo ya wandaaji.
Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zinatarajiwa kufanyika Jumapili
ya Februari 27, 2022, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(MoCU), ambapo zimeandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Company Limited na
kuratibiwa na wadau wa hapa nchini kampuni ya Executive Solutions
Limited.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...