Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akikabidhiwa zawadi ya picha na Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo tarehe 09/02/2022 Wilayani Bagamoyo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Chuo cha Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) leo Februari 9,2022,pichani kushoto ni Katibu Mkuu Dkt Hassan Abbas
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Abdallah akizungumza mara baada ya
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa kutembelea
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo tarehe 09/02/2022
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Watumishi waTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo tarehe 09/02/2022 Wilayani Bagamoyo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akikitazama moja ya kifaa cha muziki (kinanda) kilichopo studio za TaSUBa mara baada ya kutembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo Februari 9,2022 Wilayani Bagamoyo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Said Yakub na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah, wakiongozwa na Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye wakiangalia vifaa vilivyopo studio ya TaSUBa mara baada ya kutembelea taasisi hiyo leo tarehe 09/02/2022 Wilayani bagamoyo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kuhusu uwepo wa Studio na ufanyaji kazi katika Chuo hicho mara baada ya kutembeleao Chuo hicho leo Wilayani Bagamoyo.
====== ===== ====== =======
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa, amezitakaa taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo hasa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kujiepusha na masula ya Rushwa, Uvivu, ubadhirifu na upendeleo kwenye tasnia ya sanaa ili kuweza kukuza sanaa nchini na itambulike kimataifa.
Ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kuona mikakati inayoendelea kufanyika katika taasisi hiyo na kuitaja kuwa ni taasisi ya kimkakati kwa Taifa. Aidha Waziri Mchengerwa ameahidi mageuzi makubwa ndani ya taaisis hiyo huku akitoa jukumu la kushirikiana na wadau kufanya utafiti wa falsafa ya muziki wa Tanzania (Tanzanian sound/beat).
Mchengerwa amesema kulingana na kauli ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu kutafuta vijana wenye vipaji katika sanaa mtaa kwa mtaa, anategemea TaSUBa kusaidia kuwabaini vijana wenye vipaji na kuwasaidia.
Amesema Wizara inajipanga kuhakikisha taasisi hiyo inakuwa na Televisheni yake ambayo kukiwa na matamasha ya Utamaduni na Sanaa au matangazo mbalimbali yanayohusu sanaa yawe yanarushwa moja kwa moja kwenye televisheni hiyo.
Hata hivyo amesema suala la Rushwa, uzembe na upendeleo ataendelea kupiga vita kwa maana yanashusha thamani na kuturudisha nyuma kama taifa, kila jambo linawezekana tunaweza tukashiriki mashindano makubwa ya kimataifa kama tutaamua. Pamoja na hayo Mchengerwa amesema wapo katika mkakati wa kunzisha shule za michezo nchini ambazo zitakuwa daraja la kuinua vipaji vya michezo kwa vijana wa kitanzania mbao wapo mtaani.
"Tumekubaliana na watendaji kwamba tunakwenda kuanzisha shule 56 za michezo nchini ambapo shule moja itakuwa hapa Bagamoyo kwasababu ya mazingira lakini tutajipanga namna ya kufanya ili kuboresha baadhi ya viwanja vyetu ikiwemo kiwanja cha Mwanakalengwe kilichopo wilayani Bagamoyo".
Amesema Katika ziara hiyo Waziri Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Mhe.Said Yakub Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Abdallah.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...