Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katibu
wa baraza la walei kanisa la Roman Katoliki kigango cha Parokia ya
Makambako jimbo la Njombe mashariki Dickson Myamba (48) amekutwa ameuawa
kwa kukatwa katwa na mapanga katika duka lililopo ndani ya kanisa
hilo.
Waumini wa kanisa
katoliki Parokia ya Makambako mkoani Njombe wamejikuta katika kiiza
kinene na sintofahamu baada ya usiku wa februari 7 kukuta mwili wa
Nickson Muyamba aliyekuwa katibu wa baraza la walei kigango cha
Makambako ndani ya duka la vitabu vya kiimani akiwa amekatwa na kitu
chenye ncha kali na kisha kutenganishwa mwili wake vipande viwili.
Katika
misa ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu bikira Maria
mama wa neema parokia ya Makambako Padre Jordan Mwajombe ambaye ni
Dekanusi wa Makambako amesema mauaji hayo ya kikatili ,hayaja fanywa kwa
mpango wa mungu na kwamba yamelitia doa kanisa katoliki kwa kutendeka
katika eneo la kanisa na kwamba kanisa linakwenda kutenga siku 9 kwa
ajili ya kufanya maombi maalumu ya marehemu na kuwafichua wahusika.
"Ndugu
zangu kuna makosa mengine hata shetani anaweza akayakataa,kwamba mimi
sikumtuma huyu alyefanya haya afanye hili "alisema Padre Jordan Mwajombe
ambaye ni paroko wa parokia ya Kifumbwe
Serikali
nayo imeshiriki misa na mazishi ya mtumishi huyo wa kanisa ambaye
amepewa nafasi ya upendeleo ya kuzikwa katika viunga vya kanisa kwakuwa
ameuawa akiwa kanisani akiendelea na majukumu yake ,Ambapo mkuu wa
wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa kwaniaba ya mkuu wa mkoa
akalaani vikali mauaji hayo na kisha kueleza hatua ambazo zimeanza
kuchukuliwa kubaini wahusika wa mauaji ili kuwafikisha mahakamani.
Nao
baadhi ya waumini wa parokia hiyo akiwemo Rafaela Sanga wamemuelezea
marehemu enzi za uhai wake huku nao madiwani wa baraza la Makambako
wakieleza hatua wanazokwenda kuchukua ili kuelimisha wananchi kwa lengo
la kudhibiti mauaji.
Licha mauaji hayo kutekelezwa usiku wa kuamkia februari 8 lakini hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusika Na Tukio Hilo.
Aidha jeshi la polisi mkoa wa Njombe linaendelea na uchunguzi juu ya mauaji hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...