SHIRIKA la Bima Zanzibar (ZIC), limeishauri Kampuni ya Azam Media kuwakatia wafanyakazi wake bima za ajali wakiwa kazini, ambapo zitawasaidia kuwapa faraja na hata kulipwa fidia za janga hilo kutokana na wengi wao kupata ulemavu wa kudumu katika ajali zinazotokea .
Akizungumza Meneja Bima za kibenki wa shirika hilo, Hamida Juma wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kutoa mkono wa pole na kuwafaliji kutokana na ajali ya wafanyazi zaidi ya kumi iliyotokea Mlima Kitonga.
Hamida amesema kazi ya shirika hilo sio kutoa huduma tu ya bima, lakini inatoa na ushauri kwa wadau, ambapo miongoni mwa ushauri waliyoutoa kwa Azam Media kupita kwa Mkurugenzi Mkuu Tido Mhando ni kuwakatia wafanyakazi wao bima za ajali wakiwa kazini.
"Unakuta Mfanyakazi kapata ajali amefariki, amepata ulemavu wa kudumu au ulemavu ambao si wa kudumu, kwa hiyo bima hii itaweza kutoa fidia katika majanga haya Tunawaombea Mungu wapone haraka ili waweze kurudi kazini,"
Meneja huyo, ameongeza kuwa hawawezi kurudisha uhai kwa mtu aliefariki au kumpa kiungo alichopoteza, lakini kuwa nao karibu ni kwa sababu kuna uhusino baina yao na Azam Media na Kampuni ya Azam Group, lakini pia na wadau wao.
Kwa upande wake, Mhando amesemaa wamefarijika na ujio wa Shirika hilo (ZIC) katika ofisi yao kwa ajili ya kutoa Mkono wa pole na kuwafariji kitendo hicho ni kikubwa sana katika kuendeleza Mahusiano yao, kwa sababu imekuwa ni faraja kwao.
"Ndugu yako anapokuwa tayari kukusaidia wakati kama huu kwako ni faraja sana, hasa sisi kitu ambacho kilitupa shida ni tumejikuta kwenye majanga haya ambayo yanakuja ingawa si sana lakini yanajirudi,"
"Miaka miwili iliyopita tulipata janga kubwa kidogo hilo lilitugusa mno kiasi cha kwamba sasa hivi watu wanasema hata ukiguswa na unyasi unakuwa unashtuka, lakini wanapokuja ndugu zako kukufaliji, kukaa na nyinyi na kupeana pole unapata faraja."
Aidha,Mhando ametoa shukrani na amesisitiza kuwa ushauri waliopewa wataufanyia kazi na swala la kukata bima za ajali linazungumzika, kwa hiyo wamelipokea na watalifanyia kazi suala la wafanyakazi kuwa na bima za ajali wakiwa kazini.
Meneja Bima za Kibenki wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Hamida Juma akimkabidhi Mkono wa pole Mkurugenzi wa Azam Media Jijini Dar es salaam Kwa ajali iliyotokea katika Mlima wa Kitonga Mkoani Iringa Kwa Wafanyakazi takribani 10 walionusurika kifo wakati wakiwa kazini kuelekea Mbeya Kwa ajili ya kurusha Mubashara ligi kuu.
Meneja Bima za Kibenki wa Shirika la Bima la Zanzibar ( ZIC) Hamida Juma akifafanua na kusisitiza wafanyakazi kukatiwa Bima ya ajali Ili kuweza kuwasaidia wakati wanapofikwa na Matatizo hususani ajali wawapo kazini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...