NA BALTAZAR MASHAKA,Mwanza

HALMASHAURI ya Wilaya ya Magu,imepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kwa kutekeleza vizuri mradi wa jengo la utawala na kuiagiza serikali kuipatia fedha za kuukamilisha.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa kamati hiyo jana,Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Aloyce Kwezi,alisema halmashauri hiyo ipewe fedha za kukamilisha mradi huo uweze kuwahudumia wananchi na kuwanufaisha.

“Naibu Waziri tumeridhishwa na ujenzi wa mradi huu, umetekelezwa vizuri, kamati inaiagiza serikali itoe fedha waukamilishe kwa maslahi ya wananchi wa Magu,”alisema Kwezi.

Kwa upande wake,Mbunge wa Mlalo (CCM) Rashid Shangazi aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Magu,kwa kutekeleza mradi huo kwa weledi,kwa viwango na ubora kulingana na thamani ya fedha.

“Niwapongeze Magu kwa dhati mmefanya vizuri,miaka 10 bila kukamilika lakini bado liko kwenye viwango na ubora ule ule,kwa sababu mna Mhandisi Mshauri mzuri,sisi kazi yetu ni kuisimamia serikali,tutamsaidia mbunge wenu mradi kulisemea hili bungeni kuwa kuna model nzuri Magu,”alisema.

Mbunge huyo pia alikipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa ilani na kuwezesha kazi za maendeleo kufanyika kwa weledi.

Aidha Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais(TAMISEMI), Festo Dugange alisema mradi huo ulichelewa kukamilika sababu ya changamoto ya mkataba kati ya mkandarasi na halmashauri, zimefanyiwa kazi na sasa mradi unakamilishwa na SUMA JKT hivyo maagizo ya kamati wameyapokea.

Awali Wilbard Bandolla (mchumi),kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Fiderica Myovella, aliieleza kamati wanahitaji kiasi cha sh.bilioni 2.8 kukamilisha mradi huo ulianza mwaka 2013 chini ya mkandarasi Beijing Construction Engineering Group kwa mkataba wa sh.bilioni 1.416 fedha ambazo alilipwa zote awamu ya kwanza.

Alisema mradi huo umechelewa kwa miaka 9 bila kukamilika sababu ya ukosefu wa fedha na ufinyu wa bajeti kutokidhi mahitaji ya ujenzi ambapo mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri ilivunja mkataba wa awamu ya pili ya ujenzi baada ya mkandarasi kushindwa kuendelea na kazi akitaka kulipwa fedha kabla,kinyume na taratibu za mikataba ya serikali ambayo malipo hufanyika baada ya kazi kukamilika.

Bandolla alisema kabla ya mkataba huo kusitishwa yalifanyika maridhiano kati ya mkandarasi na halmashauri kwa kupima kazi zilizofanyika na alilipwa sh.bilioni 1.8 kutokana na kuongezeka kazi ya kujenga ngazi mtambao,nguzo na hiden beem.

“Tunaomba sh.bilioni 2.8 za kukamilisha jengo la ofisi,uzio na kazi za nje za kusawazisha eneo lianze kutumika,tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Jemedari,Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya kufanyia kazi watumishi wa umma,”alisema.

Mchumi huyo alifafanua kuwa mradi huo unakamilishwa na kampuni ya SUMA JKT baada ya kufunga mkataba wa sh. milioni 132.200 na imelipwa sh. milioni 91.9 kusubiri kazi ya kuweka kingo za maji,kupiga lipu na kupaka rangi zitakazofanyika mwishoni.

Alisema awamu ya pili ya mradi halmashauri ilifunga mkataba wa sh.milioni 113.07 na Mtaalamu Mshauri MELLOW ARCHITETS,yalifanyika malipo ya sh. milioni 122.13 yakijumuisha sh. milioni 9.052 ambazo hazikulipwa awamu ya kwanza,pia sh.bilioni 2.056 zilipokelewa na sh. bilioni 2.014 zilitumika kumlipa mkandarasi pamoja na mtaalamu mshauri.

Awamu ya tatu halmashauri imesaini mkataba na SUMA JKT wa sh.milioni 917 kujenga kuta,kuezeka eneo la wazi la katikati ya jengo na kufunga lenta,imeingia mkataba na MELLOW ARCHITECTS wa sh. milioni 82.5 na kazi zimefanyika ambapo mkandarasi amelipwa sh.884.8 na kufanya jumla ya sh.milioni 967.3. Kwa mujibu wa Bandolla mradi huo ulitarajiwa kugharimu sh. bilioni 7.5, zimeshatumika sh.bilioni 4.5 ambapo wakandarasi wamelipwa sh.bilioni 4.2 na mtaalamu mshauri sh.milioni 287.9 kwa awamu tatu zote za mradi

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),wakipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Magu,kutoka kwa Mhandisi Gisbert Mlelwa (wa nne kutoka kushoto),kutoka kulia wa nne ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Festo Dugange na wa tano kutoka kulia ni Mbunge wa Mlalo (CCM)Rashid Shangazi.Picha na Baltazar Mashaka

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Festo Dugange (kulia) na Rashid Shangazi wakipanda ngazi kukagua mradi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Magu,wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ilipotembelea mradi huo jana.Picha na Baltazar Mashaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...