Na Mwamvua Mwinyi-
Dkt.
Joseph Chacha Sunguro wa hospitali ya CCBRT akimpima macho mmoja wa
wakazi wa Kunduchi, Dar es Salaam katika zoezi la uchunguzi wa afya ya
macho na magonjwa ya mifupa lilioendeshwa kwa pamoja katika ya hospitali
ya CCBRT na kituo cha afya cha Jeshi la Polisi Kunduchi.
Zaidi
ya wakazi 100 wa Kunduchi wamepatiwa huduma hiyo. Tangu mwaka 2020
taasisi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana ili kuwa na nguvu ya pamoja
katika kutoa huduma za afya kwa watanzania wenye mahitaji. Kazi ya
Jeshi la Polisi ni zaidi ya kuwalinda raia na mali zao inakwenda mbali
kuwalinda kiafya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...