Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amefanya ziara ya kushtukiza katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu kilichopo mkoani Morogoro na kukagua miundombinu ya chuo hicho, changamoto walizonazo na namna kinavyojiendesha.
Akiwa chuoni hapo IGP Sirro pia alizungumza na baadhi ya askari Polisi wanaosoma kozi ya Astashahada na Stashahada ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na kuwataka wanafunzi hao kuzingatia masomo wanayofundishwa kwa lengo la kwenda kutoa huduma bora kwa wananchi na kutangaza taswira njema ya Jeshi la Polisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...