Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya Nmb, Filbert Mponzi (wa tatu kulia) akibonyeza kitufe kuashiria kuchezesha Droo ya mwisho ya msimu wa tatu wa Kampeni ya NMB MastaBata Kivyako Vyako. Kutoka kushoto ni Meneja NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi Benki ya NMB, Aikansia Muro na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga, (kulia) ni Meneja Mwandamizi kitengo cha Kadi, Manfredy Kayala na Balozi wa Kampeni hiyo, Masoud Kipanya.

**********************

MIEZI mitatu ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ iliyoendeshwa na Benki ya NMB, imefikia tamati leo kwa wateja 30 kujinyakulia kitita cha Sh. Mil. 90 (sawa na Mil. 3 kila mmoja), hivyo kukamilisha kinyang’anyiro kilichobeba zawadi ya pesa taslimu Sh. Mil. 240.

Hitimisho ‘Grand Finale’ la kampeni hiyo, limefanyika NMB Tawi la Sinza jijini Dar es Salaam, kufikia ukomo kwa mchakato uliowanufaisha wateja 1,080, kati yao 1,000 wakijinyakulia Sh. Milioni 100 (sawa na Sh. 100,000 kila mmoja), huku 50 wakitwaa Sh. Mil. 50 (sawa na Mil. 1 kila mmoja) na 30 wa fainali wakishinda Mil. 90 hizo.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi, alisema malengo ya kampeni hiyo, ambayo ni kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu, yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kumekuwa na ongezeko la asilimia 10 ya watumiaji wa kadi.

Huu sio mwisho, kampeni hizi zitaendelea na tutaendelea kutoa elimu kwa jamii itambue umuhimu wa kutumia kadi badala ya pesa taslimu, kwa sababu ni rahisi, nafuu na salama zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...