JAJI Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma ameeleza kuwa aliyekua Rais wa awamu ya tano, Dk John Magufuli alimuagiza aliyekua Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi kuwapatia Mahakama kiwanja ili waweze kujenga Ofisi za Makao Makuu ya mhimili huo.

Prof Ibrahim ameyasema hayo jana wilayani Chato Mkoani Geita wakati wa kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Hayati Dk Magufuli ambacho kilitokea Machi 17 mwaka 2021.

Akizungumza na viongozi na wananchi waliojitokeza katika Misa hiyo, Jaji Mkuu amesema Hayati Dk Magufuli alimuita ofisini kwake kumuuliza Mpango wa Mahakama kuhamia jijini Dodoma na ndipo alipomtaka Mkurugenzi wa Jiji Kunambi kuwezesha upatikanaji wa kiwanja kwa ajili ya kujenga Ofisi hizo.

" Nakumbuka Mahakama ilikua Muhimbili wa mwisho kuhamia Dodoma, Bunge lilishatangulia halafu Serikali ikafuata, Siku moja Hayati Dk Magufuli akaniita ofisini kwake akaniambia Nchi imehamia Dodoma nyie Mahakama mna Mpango  gani? Nikamwambia sisi tunategemea kuwezeshwa ndio tuhame.

Ndipo akamuagiza Mkurugenzi wa Jiji ambaye Sasa hivi ni Mbunge, Godwin Kunambi ambaye alitafuta maeneo mawili makubwa kwa ajili ya ujenzi wetu. Tunashukuru tuliwezeshwa na leo jengo limefikia sehemu nzuri Sana," Amesema Jaji Mkuu Prof Ibrahim.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...