Na Mwandishi Wetu
MSANII maarufu Jaquiline Wolper, ameteuliwa kuwa balozi wa bidhaa za EMINA zinazozalishwa na kampuni ya Bingwa Laboratory ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kutambulishwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 3, 2022 Wolper aliyembatana na mume wake Richard Samwel, amesema hiyo ni fursa kwake huku akiishukuru kampuni hiyo.
Msanii huyo atapeperusha bendera ya EMINA katika kampeni ya USAFI NI AFYA awamu ya pili ambayo imezilenga shule za msingi, sekondari na vyuo vilivyoko katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo elimu na bidhaa za usafi zitatolewa bure.
Aidha Wolper ameahidi kuwa balozi mwema wa kampuni hiyo na kuwataka wasanii wanapopewa kazi kama hizo za kuwa mabalozi wa bidhaa kufanya kazi kwa uaminifu na kwa uadilifu ili waendelee kuaminiwa kwenye kazi hizo.
Pia ameahidi kuwa balozi mwema wa kampuni hiyo na kushiriki katika kampeni ya usafi Mkoa wa Dar es Salaam ambapo watagawa vifaa mbalimbali vya usafi kwa vyuo vikuu, shule za msingi na sekondari
“Ndugu zangu nimewaita hapa kuujulisha umma wa watanzania na mashabiki zangu kwamba kuazia leo mimi ni balozi wa bidhaa za EMINA na nitapeperusha bendera ya bidhaa hizi katika kampeni ya usafi ni afya,” alisema Wolper na kuongeza
“Haya mambo mazuri ya kusaidia jamii yanayofanywa na makampuni ya Bingwa Laboratory ndiyo yamenivutia mimi kuwa balozi wa bidhaa za usafi za EMINA hivyo nawaomba tuungane katika kampeni hii ya EMINA USAFI NI AFYA ambapo elimu na bidhaa mbalimbali za usafi zitatolewa bure,” alisema
Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Emmanuel Mwambete amesema awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ya usafi ni afya ilizinduliwa na Meya wa jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto mwaka jana Kivukoni.
Amesema kampeni hiyo imewalenga mama na baba lishe, madereva na makondakta wa daladala, bajaji na wauzaji wa samaki ambapo walipewa elimu ya usafi na bidhaa za usafi zilizotolewa na kampuni hiyo bure.
Balozi wa bidhaa za EMINA msanii Jaquiline Wolper akiwa ameshika bidhaa hizo wakati wa hafla ya kumtambulisha kama balozi wa kampuni ya Bingwa Laboratories atakayepeperusha bendera ya kampuni hiyo kwenye kampeni yake ya usafi kwenye shule na masoko mbalimbali. Kushoto ni mume wake Richard Samwel na kulia ni Hussein Janowalla na Emmanuel Mwambete wakurugenzi wa kampuni hiyo ya Bingwa.

Msanii maarufu Jaquiline Wolper akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi iitwayo EMINA USAFI NI AFYA ambapo shule mbalimbali zitapewa bure vifaa vya usafi na kampuni ya Bingwa Laboratory. Anayefuata ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bingwa Emmanuel Mwambete na Husseon Janowalla kutoka kampuni hiyo
3 Balozi wa bidhaa za EMINA msanii Jaquiline Wolper akiwa ameshika bidhaa hizo wakati wa hafla ya kumtambulisha kama balozi wa kampuni ya Bingwa Laboratories atakayepeperusha bendera ya kampuni hiyo kwenye kampeni yake ya usafi kwenye shule na masoko mbalimbali. Kushoto ni mume wake Richard Samwel na kulia ni Hussein Janowalla na Emmanuel Mwambete wakurugenzi wa kampuni hiyo ya Bingwa.
4. Balozi wa bidhaa za EMINA msanii Jaquiline Wolper akikata utepe kuzindua kampeni ya EMINA USAFI NI AFYA ambapo shule na vyuo mbalimbali vitapewa vifaa vya usafi bure kwa ajili ya kufanya kampeni hiyo

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...