






**************
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa Wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayojishughulisha na Masuala ya Maji Barani Afrika (Global Water Partnership – Southern Africa and Africa Coordination Unit – (GWPSA – Africa)) ameshiriki katika Mkutano wa Kimataifa Kuhusu Maji (World Water Forum) Mjini Dakar nchini Senegal.
Akiwa Dakar, Mheshimiwa Rais Mstaafu amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Macky Sall, Rais wa Jamhuri ya Senegal, Ikulu ya Senegal, ambapo wameongelea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji safi, salama na toshelevu Barani Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...