Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 27 Machi 2022 anatarajia kuondoka nchini kuelekea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani.
Pamoja na mambo mengine, Jukwaa hilo lina lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana mbinu za kuimarisha utendaji wa serikali. Mashirika ya kimataifa pamoja na wataalamu wa sekta mbalimbali kutoka nchi zaidi ya 190 wanatarajia kushiriki Jukwaa hilo litakalofanyika tarehe 29 na 30 Machi 2022.
Franco Singaile
Msaidizi wa Makamu wa Rais - Habari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...