Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

Mbunge wa Jimbo, la Kibaha Mjini Silvestry Koka amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Ujenzi wa Kituo Cha Afya Kongowe ,kitakachogharimu Tsh Mil .400 hadi kukamilika kwake.

Akiwa katika eneo la tukio, Koka amezisisitiza kamati za usimamizi wa Ujenzi huo kuwa wazalendo na kuheshimu pesa ya serikali huku akihimiza miradi kukamilishwa kwa wakati lengwa.

Hata hivyo amewataka wajumbe wa kamati hizo na Viongozi kusimamia Ujenzi sambamba na kuzingatia thamani ya pesa. 

Koka alieleza, kituo hicho kinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Kibaha, ambapo kinatarajiwa kukamilika Julai Mwaka huu na kuwanufaisha wakazi wa kata ya Kongowe na maeneo jirani.

Pamoja na hilo, alialikwa katika Mkutano Mkuu wa CCM kata ya Kongowe kuwa Mgeni rasmi na amewapongeza Viongozi wote wanaomaliza muda wao, na kuwahamasisha wanachama  wenye nia wagombee kwa uadilifu Ili kuendelea kukijenga na kukiimarisha chama .

Vilevile amegawa vyeti kwa wanachama na Viongozi mbalimbali wa kata hiyo waliofanya kazi za chama vizuri, akiwemo diwani viti maalum Kibaha, Lidya Mgaya, vyeti ambavyo vilivyoandaliwa na Kamati ya siasa ya kata hiyo ,:;Pia Koka amekabidhi viti 25  vya plastiki vyenye thamani ya Tsh 450,000/- kwenye mradi wa Vijana wa kata hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...