Tunarudisha Kwenye Jamii
Inayotuzunguka.
Meridianbet
kwa kushirikiana Emmanuel Mkuchu (muandaaji wa Meridianbet Mkuchu
cup) pamoja na Taasisi ya Bega kwa Bega
na Mama, walishirikiana kuandaa
matembezi ya hisani yaliyoambatana na ufanyaji usafi wa zahanati ya Kunduchi ikiwa
ni pamoja na kutoa vifaa tiba na vifaa vya usafi wa ndani na nje ya zahanati
hiyo.
Zoezi hilo lililofanyika Februari 26, 2022, lilihuduliwa na viongozi mbalimbali
wa eneo la Kunduchi akiwemo Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Mtongani, Bwana Tabu Athumani pamoja na Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Kilongawima, Bwana Emmanuel Mkuchu.
Akiongea na waandishi wa habari, Bwana Tabu Athumani alisema, “Kwa dhati kabisa nimshukuru mwanzilishi wa
hili wazo la kufanya hisani hii ndani ya zahanati iliyopo katika eneo langu
lakini kubwa zaidi, Meridianbet
kwa kuhakikisha inasaidia vifaa hivi vya usafi kwenye zahanati yetu
inayohudumia karibu kata nzima ya Kunduchi. Ninawatakia heri kwenye kukamilisha
mashindano yenu hapo badae na Mungu awatangulie”
Afisa
Masoko wa Meridianbet Tanzania, Bwana Twaha Ibrahim amesema, “lengo la Meridianbet ni kuijulisha jamii kuwa michezo ni fursa kwa
vijana na chachu ya ushirikiano na wao (Meridianbet)
wapo tayari kuwa sehemu ya kuhamasisha na kuhakikisha michezo inakua sehemu ya
kipato kwa vijana na jamii kwa ujumla” .
Meridianbet
Mkuchu Cup
imechukua taswira hii kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya kata ya Kunduchi
na sehemu mbalimbali za Dar es salaam.
"Vijana ni nguvu kazi ya
taifa, na wanavipaji sana lakini, baadhi yao bado hawajaonekana vyema kwenye
tasnia ya soka. Michuano hii inawapa nafasi ya kuonekana kwa jamii na kujipatia
fursa ya ajira. Pia, hii ni burudani kwa wananchi wanaohudhuria michuano
hii." Alizungumza Emmanuel Mkuchu, Mwenyekiti wa Serikali
ya mtaa wa Kilongawima, ambaye ni mratibu wa michuano hii kwa kushirikiana na Meridianbet.
Fainali
ya michuano hii ilifanyika Februari 26, 2022 ambapo ilihudhuriwa na Meya
wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Songolo Mnyonge ambapo, Tanga Boys waliibuka washindi na walijishindia pikipiki aina ya Tvs King yenye thamani ya shilingi
millioni 2.6 na kukabidhiwa zawadi yao na mgeni rasmi. Mshindi wa pili walikua
ni Nondo FC ambao walijishindia
Milioni 1 taslim, wakati mchezaji bora wa mashindano hayo akipata shilingi laki
1.
Meridianbet Pekee, Mabingwa Ndio Nyumbani Kwao!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...