ZAIDI ya Vijana 200 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano maalumu la mazingira lijulikanalo kama 'Youth Environmental Assembly' (YEA) na kuandaliwa na Taasisi ya Global Youth Parliament (GYP) kwa kushirikiana na zingine 15.

Kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Machi 10 Mwaka huu Jijini Dar es Salaam,  litafunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Seleman Jaffo, na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya mazingira.


Kwa mujibu mratibu wa Kongamano hilo Usman Mchinja, Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 Duniani kote zinazofanya kongamano hilo ambalo lengo lake kuu ni kujadili changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za kimazingira.

"Tayari maandalizi kwa ajili ya kufanyika kwa kongamano hilo yameshakamilika na kwa sasa kinachosubiriwa ni siku ya kufanyika kwake, tunashukuru kwa hatua hii kwa kuwa Tanzania ndiyo mara yake ya kwanza kuandaa mkutano huu kwa vijana" alisema Mchinja

Kimsingi alisema kongamano hilo lenye Kaulimbiu isemayo ' uwezeshaji vijana katika ushiriki wa masuala ya mazingira na hali ya hewa' matarajio washiriki wake baada ya kongamano hilo watakuwa wamejengewa uwezo wa kun'gamua changamoto zote zilizopo katika eneo hilo.

Mbali na hilo pia alisema kupitia mkutano huo, makundi shiriki hususani vijana na watoto baadae wataweza kuwa mabalozi wazuri wa mazingira kwa kuipeleka elimu hiyo mitaani na hivyo kutanua wigo wa elimu hiyo katika jamii.

Alisema mkutano huo ambao pia utafanyika kwa njia ya mtandao, mada mbalimbali zinazohusi umuhimu wa utunzaji mazingira zitatolewa kupitia wataalamu na mabalozi wa mazingira waliopo nchini.

" Malengo makuu ni kuelimisha na kujenga uelewa kwa jamii ya kimataifa na kikanda juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira ambapo kwa kulitekeleza hilo Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la Mazingira(UNEA)limekuwa likisisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira" alisema Mchinja

Kwa upande wake Mratibu wa GYP Kitaifa Mansouza KINGU, alisema kuelekea katika kongamano hilo lililodhaminiwa na wadau mbalimbali wa masuala ya mazingira, wanatarajia kufanya shughuli mbalimbali za utunzaji mazingira ikiwemo upandaji miti katika baadhi ya shule zilizopo katika Wilaya ya Ubungo na Temeke.

Aidha aliizitaja baadhi ya taasisi zitakazoshiriki kongamano hilo kuwa ni pamoja na  TANZAGREEN INITIATIVE( TAGRIN) ,HUDEFO, Jielimishe Kwanza , Gov Junction na zinginezo na kusema kuwa hatua ya Tanzania kuwa moja ya nchi 20 Duani zilizopewa jukumu la kuandaa huo, ni la kujivuni kwa kila Mtanzania.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...