Mtendaji Mkuu wa Benki ya NBC Theobadi Sabi akizungumza wakati wa hafla ya Orange Concert akielezea umuhimu wa sekta ya michezo kupata udhamini,
amesema dhamira ya benki ya NBC ni kuona wanaendelea kushirikiana na Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni katika kukuza michezo nchini.

Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) imeendelea kuwathamani wanawake wa sekta mbalimbali baada ya kuwakatia bima ya afya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ itakayowawezesha kupata matibabu nchini Kote.


Bima hiyo kutoka kampuni ya Britam itawahusisha wachezaji wote wanaocheza timu ya Twiga Stars kwa muda wa mwaka mmoja.


Akizungumza wakati wa hafla ya Harambee kwa timu hiyo ijulikanayo kama Orange Concert, Mtendaji Mkuu wa Benki ya NBC Theobadi Sabi amesema dhamira ya benki ya NBC ni kuona wanaendelea kushirikiana na Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni katika kukuza michezo nchini.


Sabi amesema, tamasha la Orange Concert wameweza kudhamini na kuichangia Twiga Stars kiasi cha Milion 55 ili kufanikisha shughuli hiyo.


“Timu ya Twiga Stars imetuletea mafanikio makubwa katika michuano mbalimbali barani Afrika na hilo halina budi kupongezwa,”amesema Sabi


“Wizara yetu ina dhamira thabiti ya kukuza soka la Tanzania na sisi Benki ya NBC tuko tayari kuwa na ushirikiano nao katika udhamini ma ufadhili wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Stars,”


Kwa upande wa Meneja Mahusiano n
Kitengo cha Bima Linda Kamuzora amesema Benki ya NBC imetoa udhamini wa bima za Afya kwa wachezaji wa Twiga Stars ambapo watapata huduma katika hospitali ndani na nje ya nchi.


Kamuzora amesema, bima hiyo itapatowa kwa wachezaji wote kwa muda wa mwaka mmoja kutoka Kampuni ya Britam na italenga katika magonjwa yote ikiwemo maumivu wanapoumia uwanjani


“Tumeangalia umuhimu wa bima kwa timu ya Twiga Stars na mwaka huu tumeanza kuwapatia bima hizo ambapo watatibiwa katika hospitali mbalimbali ndani na nje ya nchi ambazo ni takriban saba Afrika na pia zitahusu Vitengo maalumu kama vile Kitengo cha Mifupa MOI,” amesema Kamuzora.


Benki ya NBC imeendelea kuonesha mchango mkubwa katika sekta ya michezo na dhamira ya kuinua soka la Tanzania sambamba na wachezaji kuwa na afya bora wakipata matibabu yanayostahili kwa wakati.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...