WANAWAKE wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatua ndoo kichwani wanawake wenzao hapa nchini.

Wameyasema hayo jana wakati waliposhiriki kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo yamehitimishwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kila tarehe 8, Machi ya kila mwaka ni siku ya Wanawake Duniani ambapo siku hiyo inakumbusha na kutafakari juu ya matokeo ya Kijamii, Kisasa na kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni ‘Kizazi cha Haki na ustawi kwa maendeleo endelevu.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani DAWASA, Rosemary Lyamuya, alisema kuwa DAWASA inaadhimisha siku hiyo kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

"Sisi kama watumishi wanawake wa DAWASA tunampongeza Rais Samia Suluhu kwani maadhimisho haya yamekuwa ya mafanikio makubwa sana kwetu kwani utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Majisafi imewezesha kumtua mwanamke ndoo ya maji,” amesema

Amesema wamefanikiwa kumtua mwanamke ndoo ya maji maeneo mbalimbali kwa kukamilisha miradi ya maji katika maeneo ya Kisarawe, Pugu, Chalinze, Mkuranga, Mbwawa, ambayo kwa kiasi kikubwa imemuondolea mwanamke changamoto ya upatikanaji huduma.

Ameongeza kuwa mafanikio yoyote yanayoonekana hapa nchini kwa kiasi kikubwa yamechagizwa na uwepo wa wanawake katika nyadhifa kubwa na muhimu za kimaamuzi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu.

WANAWAKE wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), wakipita kwenye viwanja vya Uhuru katika maadimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatua ndoo kichwani wanawake wenzao hapa nchini.
Wanawake wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), wakipita kwenye viwanja vya Uhuru katika maadimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatua ndoo kichwani wanawake wenzao hapa nchini.
Wanawake wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), wakipita kwenye viwanja vya Uhuru katika maadimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatua ndoo kichwani wanawake wenzao hapa nchini.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...