IKIWA imebaki siku moja Dunia kuadhimisha siku ya wanawake duniani Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimetoa hamasa kwa wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi kwa kuwa wao wana mchango kwenye maendeleo ya jamii.

Akizungumza na waandishi wa Habari Profesa Zacharia Mganilwa, Mkuu wa chuo hicho kwenye Semina iliyoandaliwa na NIT leo tarehe 7 Machi 2022, Mabibo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa wanawake wakiwa mstari wa mbele kwenye masomo ya sayansi jamii itapata maendeleo haraka kwa kuwa mfumo wa maisha wa jamii wanawake wamekuwa na majukumu mengi.

Profesa Mganilwa amesema kuwa majukumu ya mwanamke yanaanzia nyumbani , kazini mpaka kwenye jamii.

Ameutaja mfano wa kukosekana ugunduzi wa mashine ya kupika ugali kwa sababu wanasanyasi wengi ni wanaume.

Amesema kuwa chuo hicho wiki mbili zilizopita kimetoa timu maalum ya hamasa iliyokwenda Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara) iliyokwenda kwenye shule za mikoa hiyo kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma Sayansi.

“Tunaye mwanafunz wa kike hapa aliyepata daraja la juu la kwanza la Hesabu ambaye tukimpatia ajira hapa anapokwenda kuhamasisha wanafunzi wengine wanaona mfano nzuri, na watahamisika kuona kuwa mtaalamu wa Sayansi ni Mwanamke” amesema Profesa Mganilwa.

Ameeleza kuwa chuo hicho kina mifano mingi yenye kutoa hamasa kwa wanafunzi wa kike kusoma sayansi mathalan Mkuu wa Idara ya Komputer na Mkuu Idara ya Hesabati na Sayansi ya jamii ni wanawake .

Profesa Mganilwa Ametoa wito kwa wanafunzi wa kike kuyachukulia masomo ya sayansi kuwa ni kama masomo mengine .

Amesema kuwa 50\50 isiishie kwenye siasa mpaka kwenye masomo na mambo mengine yahusiayo maendeleo ya Sayansi.

Akizungumza kuhusu Semina hiyo amesema kuwa imeandaliwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo kazini, nyumbani, na katika jamii.

Siku ya wanawake duniani ambayo kilele chao ni kesho wanawake wanakutana kubadilshana uzoefu na kujitathimini michango yaokwenye jamii “ amesema Profesa Mganilwa.

Dk.Zainab Mshani Naibu Mkuu Fedha Mipango na Utawala wa chuo cha NIT amesema kuwa chuo hicho kimefanya Semina kwa ajili ya wanawake kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Dk. Mshani amesema kuwa kwenye Semina hiyo kutawasiliswa mada mbalimbali ikiwemo matatizo ya afya ya akili, na masuala ya kiuchumi.


Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa.Zacharia Mganilwa akizungumza wakati akifungua semina fupi kwaajili ya watumishi wanawake wa Chuo hicho leo tarehe 07/03/2022 ikiwa ni katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.

Mkuu wa Idara ya rasilimali watu wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Joyce Bakari akizungumza wakati wa semina fupi iliyoandaliwa na NIT kwaajili ya kutoa elimu kwa Watumishi Wanawake wa Chuo hicho kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka.

Naibu Mkuu Fedha Mipango na Utawala wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt.Zainab Mshana akizungumza wakati wa semina fupi iliyoandaliwa na Chuo hicho kwa ajili ya kupeleka elimu kwa Watumishi Wanawake wa Chuo hicho kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, (NIT) Profesa Zacharia Mganilwa akicheza Muziki na wanawake wa Chuo wakati wa semina fupi iliyoandaliwa na NIT kwaajili ya kutoa elimu kwa Watumishi Wanawake wa Chuo hicho kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof.Zacharia Mganilwa wa katikati waliokaa akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wanawake wa Chuo hicho leo tarehe 07/03/2022 wakati wa ufunguzi wa semina fupi kwa ajili ya watumishi hao kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...