Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Wami Mkoani Pwani. Daraja hilo lenye urefu wa Mita 510 pamoja na barabara unganishi linajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 67 na linatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2022.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Wami, mkoani Pwani.

Mkandarasi wa Kampuni ya Power Construction Corporation Limited ya China akimweleza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa hatua za ujenzi wa Daraja la Wami, wakati Waziri huyo alipokagua maendeleo ya ujenzi huo mkoani Pwani. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage na Mkandarasi Kampuni ya Power Construction Corporation Limited ya China wakati alipokagua maendeeleo ya ujenzi wa Daraja la Wami, Mkoani Pwani.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Watumishi wa  Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani, kuhusu uadilifu na ubunifu katika utendaji mara baada ya  kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Wami, Mkoani Pwani.

(PICHA NA WUU)

………………………………………………….

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage kumsimamia kikamilifu mkandarasi anayejenga Daraja la Wami na barabara unganishi kampuni ya Power Construction Corporation Limited ya nchini China ili akamilishe ujenzi huo ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza mara baada kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75.7 Prof. Mbarawa amesema kazi zilizobaki zifanyike usiku na mchana ili ujenzi huo  ukamilike haraka na kwa viwango vilivvyokusudiwa.

“Daraja hili lenye urefu wa Mita 510 na barabara unganishi zenye urefu wa Kilomita 3.8, vyote vikamilike ifikapo Julai mwaka huu’ amesisitiza Waziri Prof Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa amesema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa wakati kwa miradi yote inayoendelea  nchini ili kuwawezesha wakandarasi kukosa visiingizio vya kuchelewesha miradi nchini na kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa zinazoletwa na miradi hiyo.

“Tumejipanga kuhakikisha miradi yote ya ujenzi wa barabara, mdaraja na vivuko inayoendelea inakamilika kama ilivyokusudiwa, hivyo wote mliopata bahari ya kusimamia miradi hiyo fanyeni kazi kwa uzalengo ilikupata thamani ya fedha”amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu kwa namna anavyowezesha miradi ya kimmkakati ya WIzara ya Ujenzi na Uchukuzi kutekelezwa na kuitaja miradi hiyo kuwa ni Barabara ya Bagamoyo-Pangani Tanga hadi Lamu, Daraja la Kigongo-Busisi, barabara ya mzunguko mkoani Dodoma, Viwanja vya ndege vya Msalato, Mtwara, Musoma, Songea na Iring ambayo ikikamilika itaibadili sura ya Tanzania kiuchumi na kijamii.

Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage amesema ujenzi wa daraja jipya la Wami lenye upana wa kuwezesha magari mawili kupishana  kwa wakati mmoja utaondoa adha ya daraja la zamani lililojengwa mwaka 1959 ambalo haliendani na mahitaji ya sasa.

Mhandisi Mwambage amesema daraja jipya litapunguza ajali na msongamano katika barabara ya Chalinze hadi Segera na hivyo kuongeza tija kwa watumiaji wa barabara hiyo.

“Faida nyingine tunayoipata kutokana na mradi huu ni kuwezesha wataalam wetu kupata utaalam wa kujenga madaraja makubwa ya kiwango hiki na zaidi ya wafanyakazi 400 wamepata ajira kulipitia mradi huu” amesema Mhandisi Mwambage.

Ujenzi wa daraja la Wami ni mwendelezo wa mikakati ya Serikali ya kufungua barabara kuu ili kuwezesha huduma za usafiri na uchukuzi kuwa za uhakika na zinazoaminika na hivyo kuvutia wawekezaji na kurahisisha huduma za uchukuzi nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...