Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka viongozi wa ngazi mbali mbali kujitahidi kusimamia vyema majukumu yao kwa vile kukubali wenyewe na kuahidi kuwatumikia watu.

Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo katika ziara yake ya kichama kuyatembelea majimbo ya Kijini na Nungwi mkoa wa Kasikazini Unguja.

Amesema viongozi wote kuanzia wa Matawi, Majimbo , Mikoa hadi Taifa wanawajibu wa mkubwa wa kuhakikisha wanashirikiana vyema na wananchi na kusimamia ipasavyo majukumu yao na huko ndiko kutakakowafanya wananchi na wananchama kujenga imani na viongozi ya kupata matarajiuo yao ya kuwachagua.

Akizungumzia suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Mhe. Othman, amesema kwamba chama hicho kimeingia katika serikali hiyo ili kusaidia kujenga na kutengeneza kwa pamoja mfumo bora wa kuendesha nchini.

Amefahamisha kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa itasaidia sana kuetengeneza mazingira sahihi ya ushirikiano wa kuleta mageuzi katika mfumo kuendesha serikali ya Zanzibar na kwamba chama hicho tayari kimewasilisha mapendekezo kadhaa serikani ikishauri kuwepo mabadiliko ya maeneo mbali mbali, likiwemo suala utaratibu wa uchaguzi.

Akizungumzia suala la Sensa ya watu na Makaazi inayotarajiwa kufanyika Ogasti mwaka huu, Mhe. Othman amesema ni jambo muhimu na kuwataka wananchi wote wasipuuze jambo hilo na kuwa tayari kuhesabiwa muda utakapowadia.

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho wa Jimbo la Kijini ndugu Mcha Khamis, amewataka wanachama wa chama hicho kuendelea kushirikiana kuimarisha chama kwa kuunganisha wanachama wapya kama muongozo wa chama hicho unavyoelekeza.

Mapema katika ziara hiyo Mhe. Othman aliweka mawe ya msingi ya Matawi mapya matatu ya Jimbo la Kijini pamoja na kuzindua tawi jipya la Mwanahayanza huko Matemwe Kigomani pia alitembelea na kusikiliza wananchi wenye mgogoro wa aridhi ulipo baina yao na muekezaji huko Mbuyu Tende Matemwe na kuahidi kwamba ataliwasilisha kwa mhe. Rais jambo hilo ili lipatiwe ufumbuzi.

Nao Wananchi wa mbuyu Tende Matemwe wamelelamikia vitisho wanavyopewa na serikali ya Mkoa ikiwataka wasiendelee kudai haki yao ya aridhi aliyopewa muwekezaji bila ridhaa zao.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...