Na Khadija Kalili, Kibaha

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amemwagia sifa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameonyesha nafasi na uwezo wa Mwanamke duniani kutokana na uwezo wake mkubwa ameonyesha katika kuwajibika.

Amesema hayo wakati akizindua siku ya Wanawake duniani kimkoa katika viwanja vya Mailimoja mjini Kibaha na kuhudhuriwa na akinamama kutoka mkoa mzima wa Pwani.

Alisema hata wale ambao walikua na mashaka juu ya uongozi wa mwanamke kwa sasa kutokana na namna anavyoupiga mwingi hawana la kusema hivyo wanawake wote tembeeni kifua mbele kwani tunaye Kiongozi imara na madhubuti mwenye jinsia ya kike. 

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa amewataka wadau wote wanaojishughulisha na masuala ya malezi ya watoto wa kike wakajifunze kwenye shirika lisilokuwa la kiserikali la Room to read ambalo linamuhudumia mtoto wa kike katika shule za msingi na sekondari za serikali kwa kutoa mafunzo ya stadi za maisha.

Alisema jinsi shirika hilo la Room to read linavyotoa ushauri, msaada wa vifaa na ushirikishwaji wa familia shule na jamii sambamba, elimu ya fedha na ujasiriamali na masuala ya usomaji na maktaba ni mbinu madhubuti katika kukusaidia moto wa kike na mwanamke kwa ujumla kujilinda hadi afikie malengo yake.

Aidha Alhaji Kunenge amewataka wanawake  wajasiriamali kujituma zaidi Ili kuweza kujikomboa kiuchumi kwa kuleta maendeleo ndani ya familia na Taifa kwa ujumla.

RC Kunenge amesema haya  leo Machi mbili katika viwanja vya Maili Moja Wilayani Kibaha  alipokuwa akizindua  sherehe za kuelekea  siku ya Wanawake Duniani ambayo itaadhimishwa duniani kote ifikapo Machi nane ambapo kwa Mkoa wa Pwani maadhimisho haya yatafanyika kimkoa katika Halmashauri ya Chalinze huku kauli mbiu  ya mwaka huu inasema  'Haki na Usawa  kwa maendeleo Endelevu'.

Mkuu huyo wa Mkoa amewaahidi wajasiriamali  hao kuwa atakutana nao Ili waweze kujadili masuala mbalimbali yanayo wahusu na siku hiyo atajaa nao kama Alhaji Kunenge huku akisisitiza kuwa wawe huru siku hiyo katika kuzungumza nae kwa kinaga ubaga.

"Tutakaa nawenzangu tuangalie namna ya kuweza kutoa mkopo wenye tija utakaomwezesha  mkopaji  kufanya jambo la maana pia tutawasaidia kuwapa mafunzo na miongozo Ili wakopaji  waweze kukopeshwa wakishafanikiwa waweze kukopeshwa wengine hili liko ndani ya uwezo wetu nitalijadili na Kamati yangu"alisemaKunenge.

Kila kikundi tutawafikia hakuna kundi au mtu atakayeachwa tutajitahidi tufungue fursa zaidi kwani njia ya kuwasaidia nyie ni kutoa fursa zaidi za kibiashara ,tuzingtie sheria na tutumie fursa.

"Tuhakikishe sisi sote tunashiriki katika sensa ya watu na makazi tujitokeze tushiriki vizuri na tupate chanjo za ugonjwa wa UVICO 19  takwimu zinaonyesha katika nchi yetu wale ambao hawajapata chanjo ndiyo wanaopata madhara zaidi" alisema Kunenge.

Katika sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali  wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usala ya Mkoa wa Pwani wengine ni pamoja na  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Pwani (UWT)Farida Mgomi ambaye alisema kuwa uzinduzi huu utaambatana na  kufanyika maonyesho ya bidhaa mbalimbali za  wajasiriamali wa Wilaya Kibaha huku akitoa wito kwa wakazi wa Wilayani hapa kujitokeza katika kuwaunga mkono.

"Alisema kuwa baada ya uzinduzi huu Machi sita kutafanyika usiku Maalumu utakaofahamika kwa jina la Usiku wa wa Mwanamke wa Pwani ambapo kutafanyika mambo mbalimbali hasa kujua Mila na desturi za Mkoa waPwani' alisema Mwenyekiti huyo.

Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani Subira Mgalu ametoa pongezi kubwa kwa Wilaya na Mkoa kuandaa sherehe hizi ambazo kilele chake ni Machi nane.

Mkuu wa Wilaya Sara Msafiri alisema kuwa mwaka huu Wilaya imejipanga hivyo wataendelea  kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kwenda kutembelea waginjwa katika Hospitali  ya Ocean Road, gereza la Mkuza ambapo baadhi ya  wanawake kutokaWilayani hapa watakwenda kutoa misaada.

"Tumejipanga kuwajengea uwezo kina mama kwa kuwapa mafunzo Maalumu Ili waweze kupanda madaraja katika biashara  zao mwisho napenda kywashukuru wadhamini wetu ambao ni NMB, TRA, OSHA,TARURA,ROOM TO READ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...