Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MRADI wa Kilimo himilivu Cha Mtama unaoendelea katika Wilaya sita zilizopo mkoani Dodoma unafadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Dunia(WFP) chini ya mfadhili mkuu ubalozi wa I erland kwa ushikirikiano wa utekelezaji wa mradi na Shirika la Farm Africa pamoja na wadau wakubwa ambao ni Serikali.
Aidha mradi huo wa kilimo himilivu wa zao la mtama uliaza mwishoni mwaka 2018 katika mkoa wa Dodoma na Wilaya ambazo zinanufaika ni Kongwa, Mpwapwa, Chamwino, Bahi, Chemba na Kondoa.
Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini vimepata nafasi ya kutembelea Wilaya hizo kwa lengo la kuona yale ambayo wakulima wa mtama wameyapata kutokana na kujihusisha na mradi huo wa WFP ambao unatekelezwa na FarmAfrica.
Kwa Wilaya ya Bahi ikiwa miongoni ya wilaya ambayo ipo kwenye mradi kupitia mtekelezaji ambao unatekelezwa na Shirika la Farm Africa tangu mwaka 2019. Dhumuni kuu la mradi huo ni kuwafika wakulima wadogo wadogo ambao wanajishughulisha na kilimo cha zao la mtama ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji yao ya kiuchumi kupitia uzalishaji wenye tija ambao utasababisha uwepo wa uhakika wa chakula, kuongeza kipato na lishe bora kwa ngazi ya kaya.
Mwandishi wa Michuzi TV na Michuzi Blog ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyopata fursa ya kutembelea miradi hiyo katika Wilaya zinazotekeleza mradi huo wa WFP na FarmAfrica.
Akizungumza na Michuzi Blog kwenye mahojiano maalum kuhusu mradi huo kwenye Wilaya ya Bahi,Ofisa Miradi kutoka Shirika la Farm Africa Grace Changamike anataja dhumuni mahususi la mradi ni kuongeza uzalishaji wenye tija,kuwa na uhakika wa chakula kwa ngazi ya kaya,kuongeza kipato kupitia uzalishaji wa ziada na kupata lishe bora kwa ngazi ya kaya.
"Pamoja na mradi huu wa kilimo himilivu cha zao la mtama shirika la Farm Africa limeweza kuwafikia wakulima wanufaika wapatao 3916 wakiwa wanaume 1989 na wanawake 1927 na kuunda vikundi vya umoja wa wakulima vipatavyo 96 katika wilaya Bahi kupitia vijiji vya mradi 47
"Vijiji hivyo ni Mwitikila, Mphangwe, Mtitaa, Nchinila, Isangha, Chibelela, Ibhugule, Mapanga, Nkhome, Nholi, Mpalanga, Chidilo, Zejele, Nondwa, Chiguruka, Chipanga A, Chipanga B, Chipokelo, Chali makulu, Chali isanga, Chali igongo, Nghulugano, Chimendeli, Mzogole, Mpinga, Kigwe, Mapinduzi, Ibhiwa, Mnkola, Ilindi, Mindola, Nguji, Chilungulu, Mundemu, Kisima cha ndege, Mchito, Tinai, Lamaiti, Bankolo, Lukali, Chonde, Makanda, Kongogo, Babayu, Mayamaya, Mkondai na Zanka,"amesema.
Kuhusu baadhi ya shughuli za mradi zilizotekelezwa kwa kipindi Cha mwaka 2021 katika Wilaya ya Bahi, Meneja huyo wa mradi huo anafafanua katika kipindi cha mwaka 2021 shughuli zilizoweza kutelezwa kupitia vijiji vya mradi ni kuimarisha,kuvijengea uwezo na kusaidia Usajili kupitia idara ya Maendeleo ya jamii.
"Mradi umeweza kujengea uwezo na kuimarisha vikundi vya wakulima vipatavyo 96 na kuweza jinsi ya kuandaa katiba ya usijali kati ya hivyo 75 vimeweza kupata usajili wa awali kupitia idara ya maendeleo ya jamii na vikundi 21 viko kwenye hatua ya kuandaa katiba.
"Pia kuwapatia Mafunzo ya kilimo bora cha Mtama ambapo mradi umeweza kuwapatia mafunzo ya kilimo bora katika nyanja ya uandalizi wa mashamba, utunzaji, uthibiti wadudu na magonjwa ya mimea, na kutumia mbegu bora za kisasa za mtama. Mradi uliweza kuwapatia mafunzo wakulima wanufaika wapatao 3916,"amesema Changamike.
Ameongeza shughuli nyingine zilizotekelezwa ni kuanzishwa mashamba ya mfano au darasa la Mtama kwa kutumia mbegu za kisasa na kwamba kupitia mradi huo wameanzisha mashamba darasa 15 katika vijiji 15 kwa msimu uliopita wa mtama kwa kutumia njia tofauti za kuonyesha wakulima ili waweza kujifunza kupitia mashamba darasa ya mtama kwa kutumia mbegu bora za kisasa .
Amefafanua lengo likiwa kuwasidia wakulima kuondokana na kilimo cha mazoea na kuiga kilimo bora cha kisasa kwa kulima eneo dogo na kupata matokeo ya mavuno mengi.Pia mradi umeweza kuwaunganisha wakulima na watoa huduma za bembejeo na vifaa vya kilimo baada ya kupata mafunzo ya kilimo bora na udhibithi na upotevu wa mazao kwa kununua maturubai imara ya kuanikia mtama.
Pia mifuko maalum ya kuhifadhia mtama baada ya kupura na kukauka vizuri kwa kiwango maalum na kununua mashine ya kisasa ya kupura nafaka ikiwemo mtama ili kuondokana na zana ya kilimo cha kienyeji na kupunguza upotevu wa mazao na uhifadhi bora na kuongeza ubora wa mtama baada ya kuvuna.
Pamoja na hiyo wakulima wameza kujipatia huduma hiyo kwa unafuu moja kwa moja mpaka vijijini na kufikia kwa mwaka huu maturubai 389, mashine 1 na mifuko 678 kuweza kununuliwa na wakulima kupitia mradi unatekelezwa na shirika la Farm Africa.
Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni kutolewa Mafunzo kwa wakulima wa kuzalisha Mbegu ya Mtama ya daraja la kuazimia kupitia Taasisi Maalum ya Udhibithi wa Mbegu Bora(TOSCI)."Kupitia mradi huu shirika liliweza kuwachagua wakulima wanne kutoka katika vijiji vya Chali igongo, Kisima cha ndege, Lamaiti na Mapanga na kuweza kushirika mafunzo maalum jinsi ya uzalishaji mbegu ya mtama la daraja la kuazimia
"Mafunzo hayo yalitolewa na Taasisi maalum ya udhibiti wa mbegu bora Tanzania (TOSCI) kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa mbegu yam tama ili kuongeza upatikanaji wa mbegu hiyo kirahisi.Pia uzalishaji wa mashamba ya Mbegu ya Mtama wa daraja la kuazimia ambapo mradi uliwezesha kuazisha mashamba ya uzalishaji wa mbegu ya tama wa daraja la kuazimia yapatao manne yenye jumla ya ekari 8 kwa ushirikiano wakulima waliopewa mafunzo jinsi ya uzalishaji wa mbegu.
"Na kuweza kufanikiwa mashamba mawili ambayo yalifunzu utunzaji bora wa uzalishaji kwa kutunza na uangalizi wa karibu mpaka kubakia ekari 3 ambazo ekari 1 ni kijiji cha Kisima cha ndege na ekari 2 kijiji cha Chali igongo na kupata kilo 708 za mbegu yam tama ya daraja la kuazimia, ingawa mashamba menginge yalishindwa kufunzu kutokana na changamoto ya usimamizi wa karibu na kupelekea kushambuliwa na ugonjwa wa fangasi na kupoteza ubora na uthibiti wa uzalishaji wa mbegu ya mtama wa daraja la kuazimia."
Aidha uwasilishwaji wa bustani wa jumla na bustani za nyumbani ambapo Grace anasema mradi umeweza kuwasidia wakulima elimu ya kuazisha bustani za jumuia na za nyumbani baada ya kilimo cha msimu ili kukidhi mahitaji ya lishe bora na kuongeza kipato kidogo kwa ngazi ya kaya, pamoja na hayo mradi umeweza kuwapatia wakulima wa 428 wakiwemo wanawake 221 na wanaume 207 mbegu za mboga mboga kama mchicha, figiri, Chinese, bamia ili waweze kuazisha bustani za nyumbani kwa ajili ya lishe bora na kuongeza kipato kidogo.
Ameongeza kuwa shughuli nyingine iliyotekelezwa ni kuanzisha mfumo mdogo wa umwagiliaji kwa wakulima walio ndani ya mradi ambapo mradi umewawezesha wakulima wawili katika kijiji cha Ibhiwa kwa kuwafungia mfumo mdogo na rahisi na wenye gharama nafuu ambao utakaowezesha kufanya kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone, dhumuni la mfumo ni kumuezesha mkulima kupata mboga mboga kwa msimu wote kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kuuza kwa wakulima wenzeke.
Pia mradi umeweza kuazisha bustani ya vitalu ya miche kwa ajili ya miti malisho aina ya Gliricidia na miche ya mipapai katika vijiji vifuatavyo; Kisima cha ndege, Babayu, Lamaiti, Lukali, Ilindi, Chiguruka, na Mindola ambayo inategeme kupata miche 4000 ya mipapai chotara, na miche 10000 ya miti malisho ambayo imewajengewa uwezo vikundi vya wanawake, vijana na mkulima mmoja mmoja kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
"Pamoja na hiyo baada ya ukuaji miche hiyo itasambazwa kwa wakulima wote ambao wapo kwenye vijiji vya mradi nia ya kuongeza uelewa juu ya kuwa na miti malisho kwa ajili kuongeza udongo kwenye rutuba na kuwa chakula cha malisho ya mifugo kama kuku, nguruwe, ng’ombe, mbuzi na kondoo, pia na kuwa mkakati wa kila kaya kuwa miti ya mipapai kwa ajili kupata matunda ili kuongeza lishe bora,"amesema.
Akizungumza kuhusu somo la kujifunza kutokana na shughuli za mradi,amesema ni uanzishwaji wa mashamba mbegi yatasaidia kuondoa upungufu wa upatikanaji wa mbegu za kisasa ya Mtama,kuanzosha bustani ya mboga manyumbani ambako kumesaidia kuongeza kiasi kikubwa cha lishe bora kwa familia na kipato.
Pia mabadiliko ya wakulima katika kutumia vifaa vya kisasa vya kuvunia, kupura na kuhifadhi mtama, ushirikishwaji wa wanawake na vijina umeongezeka hasa katika shughuli za kilimo cha bustani za mboga mboga na masoko ya kuuza mtama pamoja na upatikanaji wa soko la uhakika wa zao la mtama umeongeza muamko kwa wakulima kwa kuzalisha mtama kwa wingi.
Kuhusu changamoto anasema baadhi ya wakulima bado wamekuwa wagumu katika kutumia mbegu bora za kisasa za mtama na badala yake kuendelea kutumia mbegu za kienyeji .Pia changamoto nyingine ni uchache wa mvua kupelekea kupungua kwa uzalishaji, ushirikiano mdogo wa wakulima na wataalamu kwa ukaribu zaidi pamoja na miundombinu hasa barabara zilizopelekea wanunuzi kushindwa kuwafikia wakulima kwa vijiji vingine kipindi cha mauzo.
Pamoja na yote hayo jambo kubwa ambalo WFP na Farm Africa wanajivunia ni kuona wakulima wanaojihusisha na kilimo himilivu cha Mtama katika Wilaya ya Bahi ni mafanikio ambayo wamekuwa wakiyapata, wakulima wamepiga hatua kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...