Na Karama Kenyunko Michuzi TV

Tanzania na Afrika Kusini zimeunganisha nguvu kwa ajili ya kuwainua wabunifu wanaochipukia kwenye miradi ya Afya na Usalama wa Chakula kwa lengo la kuwainua na kujitengezea ajira.

Kufuatia muunganiko huo, vijana wametakiwa kuwa sehemu ya kufanikisha lengo hilo kwa kuwasilisha mawazo yao ya kibunifu Costech bila hofu yoyote ili kuweza kuinua fani ya Sayansi na Teknolojia na ubunifu nchini.

Mkurugenzi wa Kituo cha Uendelezaji na Uhaulishaji Teknolojia wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (costech) Gerlad Kafuku ameeleza hayo leo Machi 29,2022 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi na kampuni changa (startups) zenye mawazo bunifu yanayoandaliwa kuwa bidhaa zinazoshiriki mradi wa mpya wa Twiga unaotekelezwa na nchi za Tanzania na Afrika Kusini.

Amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa kwa miaka miwili umetengewa sh. Milioni 300 kwa ajili ya kuziendeleza kampuni changa tatu kutoka Tanzania zenye mawazo bunifu zilizo kwenye mradi huo.

Amesema wamebaini kinachowakwamisha vijana wengi kupeleka mawazo yao kwenye tume hiyo ili yaendelezwe ni kuhofia kutakiwa kuandika maandiko ya kitaalamu kitu ambacho ni tofauti na utaratibu wao...."Tutawasaidia vijana kuinua bunifu zao ambazo pia zitakuwa majibu ya changamoto mbalimbali nchini”, amesema Dkt. Kafuku.

Amesema kuwa miradi hiyo itakuja na majibu ya changamoto za uhifadhi wa mazao yasiharibike ambapo itaokoa hasara ya mavuno.

"Ninawaasa vijana wewe kama una wazo lako la ubunifu njoo Costech lilete hata kwa kuandika sentesi mbili, kama kitu kipo kitaonekana tu, hatutaki nyaraka kubwa na nyingi kama wafanyavyo maprofesa hivyo msihofie kuja na sio lazima mfike hapa mnaweza kuwasiliana na sisi kupitia ofisi yoyote ya serikali nchi nzima,” amesema Dkt. Kafuku

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa nchi ina lengo la kuhakikisha vijana wanapata ajira na lengo la kujitegemea kiteknolojia ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma hapa nyumbani hali itakayosaidia kupunguza utegemezi kutoka nje ya nchi.

Dk Kafuku ametoa wito kwa Mbunifu yeyote mwenye wazo endelevu alipeleke COSTECH watamsaidia mtaji wa kuliendeleza mpaka kufikia hatua kubwa kwa kuyakuza na kuwapatia fedha pale itakapobidi au kuwaunganisha na fursa zinazotoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, mratibu wa program ya Twiga kutoka Afrika Kusini Sina Legong amesema lengo la mradi huo ni kuunga mkono mawazo ya kibunifu katika sekta ya afya na kilimo na inahusisha kampuni changa saba kati ya hizo nne za Afrika kusini na tatu za Tanzania.

Mbali na hilo Sina amesema mradi huo utasaidia pia nchi hizo kubadilishana uzoefu kwenye bunifu mbalimbali na kusaidia nchi hizo kupata wabunifu wenye uweledi.

Amesema kuwa miradi hiyo ni mwanga wa maendeleo kwa kuwa inaibua utatuzi wa changamoto mbalimbali kwenye jamii.

Mkurugenzi wa Kituo cha Uendelezaji na Uhaulishaji  Teknolojia wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (costech) Dkt. Gerlad Kafuku, akiwasilisha azimio la ushirikiano na Afrika Kusini leo Machi 29, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi na kampuni changa (startups)  zenye mawazo bunifu yanayoandaliwa kuwa bidhaa zinazoshiriki mradi wa mpya wa Twiga unaotekelezwa na nchi za Tanzania na Afrika Kusini.
Wawakilishi wa Mradi wa Twiga kutoka Afrika Kusini na Tanzania,  wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Kituo cha Uendelezaji na Uhaulishaji  Teknolojia wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (costech) Dkt. Gerlad Kafuku, alipokuwa akiwasilisha azimio la ushirikiano la nchi hizo mbili,  leo Machi 29, 2022 jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na kampuni changa (startups)  zenye mawazo bunifu yanayoandaliwa kuwa bidhaa.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uendelezaji na Uhaulishaji  Teknolojia wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (costech) Dkt. Gerlad Kafuku, (aliyesimama nyuma katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na  Afrika Kusini leo Machi 29, 2022 jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kikao kazi na kampuni changa (startups)  zenye mawazo bunifu yanayoandaliwa kuwa bidhaa zinazoshiriki mradi wa mpya wa Twiga unaotekelezwa na nchi za Tanzania na Afrika Kusini.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...