Na Bashiri Salum, Mbeya
Tume ya Kurekebisha sheria Tanzania, imefanya tathmini ya utekelezaji wa sheria katika sekta mbalimbali zikiwemo sheria ya adhabu mbadala, sheria ya sekta ya utalii, na Sheria ya mifugo na uvuvi lengo likiwa ni kubaini changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake na kuzifanyia tathmini kama malengo yaliyokusudiwa wakati wa kutungwa kwa sheria hizo yamefikiwa.
Akifafanua leo katika kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa BOT Tawi la Mbeya katika wasilisho lililotolewa katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume Bwana Khalist Michael Luanda akabainisha kwamba tathimini hiyo imefanyika kwa kupitia sheria nyingi zinazotumika katika sekta mbalimbali ambapo Tume inatarajia kukamilisha taarifa nne (4) za tathmini ya utekelezaji wa sheria.
Aidha Kaimu Katibu Mtendaji huyo alieleza mikakati ya Tume katika kuimarisha mawasiliano kwa kutumia vyombo vya habari ili kuitangaza taasisi hiyo ambapo kwa sasa wanajipanga kuandaa na kurusha vipindi vya redio na runinga kwa lengo la kutoa elimu ya sheria kwa umma.
Hata hivyo Bwana Luanda amebainisha kwamba Tume ya Kurekebisha Sheria imejipanga kutoa elimu kupitia vyombo vya habari juu ya Ushiriki wa wananchi katika mchakato wa maboresho ya Sheria hapa nchini .
“Sheria nyingine ambazo Tume imetoa elimu ni Sheria ya Mtoto, Sheria za Ajira Tanzania, Sheria za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi na Haki za walaji”. Alisisitiza katibu Mtendaji Khalist Luanda.
Naye Mchumi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi Fatma Saidi Alawi wakati wa wasilisho lake kuhusu mikakati ya miaka mitano ya Taasisi hiyo amesema kipindi cha Julai, 2021 hadi Februari, 2022, Tume imechambua hukumu hamsini (50) za Mahakama ya Rufaa ya Tanzania na kuzibainisha Kanuni za Kisheria (Legal principles) mbalimbali zilizotumika katika kufanya uamuzi.
Aidha Bi Fatma ametoa wito kwa wadau mbalimbali wanaohitaji kutumia Kanuni hizo kutembelea tovuti ya Tume kwa ajili ya kurahisisha watumiaji kufuatilia maendeleo ya Sheria mbalimbali kupitia maamuzi ya Mahakama.
Akiendelea na wasilisho lake Bi Fatma akafafanua kwamba Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Februari, 2022, Tume imeshiriki katika kutafsiri sheria 17 zinazosimamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili.
Akimalizia wasilisho lake Bi Fatma anasema kwamba Tume imeandaa Miongozo ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi katika Mabaraza ya Kata na Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji.
Hata hivyo baraza la wafanyakazi limehitimishwa leo baada ya wajumbe kutumia siku mbili kujadili mambo mbalimbali ya kiutumishi pamoja na mikakati ya kuboresha uendeshaji wa Taasisi hiyo.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania, Bw. Khalist
Luanda akiwasilisha mada kuhusu maisha baada ya kustaafu katika Ukumbi
wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Tawi la Mbeya, katika baraza la
wafanyakazi lililofanyika leo.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania, Bw. Luanda
akieleza mikakati mbalimbali walijiowekea ili kufanikisha malengo ya
Tume hiyo.
Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakifuatilia mawasilisho mabalimbali.
Dereva wa Tume hiyo, Wense Evadi akichangia mada.
Mchumi
kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Bi Fatma Alawi
akiwasilisha mada kuhusu mikakati ya miaka mitano inayohusu maendeleo ya
Tume.
Home
HABARI
TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YAFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA SHERIA MBALIMBALI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...