OR- TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu( Afya) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Grace Magembe amesema kuanzia sasa ukaguzi wa bidhaa za afya itakuwa ni moja ya kiashiria cha ufanisi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri.
Ameyasema hayo leo tarehe 3 Machi,2022 alipofanya ukaguzi wa ubora wa utowaji wa huduma za afya katika Halmashauri ya Gairo na Mvomero Mkoani Morogoro ulioambatana na ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma ya afya inayoendelea kutekelezwa.
Dkt. Grace amesema kuwa
kutofanyika kwa ukaguzi wa dawa na bidhaa za afya kunaweza kuchangia
upotevu na matumizi mabaya ya bidhaa za afya ikiwemo dawa, vitendanishi
na vifaa tiba
Amesema kazi ya ukaguzi wa bidhaa za tiba sasa lazima ifanyike
kwa ushirikiano kati ya Idara ya Afya na Wakuu wa Idara nyingine
wakiwemo wakaguzi wa ndani.
Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kufanya ukaguzi wa bidhaa za afya kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mvomero na kuwasilisha taarifa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndani ya siku 7 kufuatia ukaguzi wa awali kuonyesha kuna bidhaa ambazo takwimu zake hazikuwa na uhalisia
Aidha, amemuelekeza Mkurugenzi huyo kuanza mara moja ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura(EMD) na kumtaka Mhandisi wa Halmashauri kutoa utaalam wa kiufundi wa namna bora ya kuweka mifereji ya kuondoa maji yanayotuama katika eneo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...