Na.Khadija Seif, Michuzi TV 

SERIKALI kwa kushirikiana na Chama cha Mchezo wa Gofu Tanzania (TGU), kimethibitisha kuwa wenyeji wa Mashindano ya Gofu " Europe Tour" yatakayofanyika Aprili 7 hadi 10 mwaka huu katika Klabu ya gofu  Kilimanjaro Jijini Arusha.

Mashindano hayo yana lengo la kuunga Mkono wa juhudi ya serikali chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan kuendeleza utalii nchini kutokana na Shindano hilo kufanyika katika Mkoa wa Kilimanjaro ambapo Kuna Mlima Kilimanjaro.

Akizungumza na Waandishi Wahabari jijini Dar es Salaam , Mwenyekiti wa TGU, Chris Martin alisema ni mara ya kwanza Tanzania kuandaa mashindano hayo makubwa ambayo yatashirikisha mataifa mbalimbali.

Aidha wachezaji 156 wamethibitisha kushiriki mashindano hayo ambapo Tanzania imetoa wachezaji 12 wa kulipwa ambapo nchi ya  Kenya, Uganda, Rwanda na Malawi kumetoa wachezaji wawili wawili.

“Hapa nchini tutakuwa na wawakilishi 12 kutoka katika klabu tofautia ambapo wote ni Wachezaji wa kulipwa na  watakuwepo wachezaji wengine kutoka bara la Ulaya, Asia na mataifa mengine nina imani mashindano haya yatatoa fursa kwa kutangaza utalii wa Tanzani,” amesema Martin.

Pia chama hicho Cha gofu (TGU) imeomba Tanzania kuandaa mashindano haya ambayo mwaka jana yalifanyika nchini Kenya yanatarajia tena kufanyika mwakani kwa mara ya pili na  kuwa wenyeji.

“Tunaendeleza kampeni ya Royal Tour ambayo Rais wetu Mama Samia ameianzisha kwa ajili ya kutangaza Utalii wa ndani na vitu vinavyopatikana hapa nchini,” alisema Martin.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Singo amesema ni jambo nzuri kuona Mashindano hayo yanatangaza utalii wa taifa, lakini serikali itakutana na Chama cha TGU kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya mashindano hayo.

“Kwa sasa hatuwezi kuzungumza lolote kwa sababu serikali tuna mpango wa kukutana na uongozi wa Chama cha gofu kwa ajili ya maandalizi ya mashindano baada ya hapo tutatoa tamko kuhusu uwenyeji wa mashindano hayo,” amesema Singo.

Katibu wa maandalizi ya mashindano hayo, Enock Magile amefafanua  sifa za wachezaji ambao watashiri lazima wawe na kiwango kizuri katika rekodi ya mchezo huo.

"watacheza ambao watakuwa na viwango hivyo watapita bila tatizo lolote lile kwa ajili ya kuitangaza taifa na kuonyesha uwezo wao.

Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa gofu nchini (TGU) Chris Martin akizungumza na Waandishi Wahabari mara baada kutambulisha rasmi Mashindano ya Mchezo wa gofu "European toru" yanayotarajiwa kuanza rasmi April 7 mwaka huu katika Jiji la Arusha likijumuisha wachezaji wa ndani na nje ya nchi Huku Wachezaji 12 wakulipwa kutoka nchini Tanzania kushiriki katika Mashindano hayo
Katibu wa Maandalizi ya Mashindano ya "European tour" Enock Magile akitolea ufafanuzi zaidi sifa za Wachezaji ambao watashiriki katika Mashindano hayo na kusisitiza kuwa lazima Mchezaji awe ni wa viwango vya juu na rekodi nzuri Kwa michezo iliyopita ambayo ameshiriki.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...