Na Farida Said, Morogoro.

SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati imesema kukamilika kwa utekelezaji wa mradi wa matumizi bora ya nishati hapa Nchini utaongeza wingi wa nishati na kupunguza gharama ya matumizi ya nishati inayotumika huku jamii ikitajwa kunufaika zaidi.

Hayo yameelezwa na Naibu Kamishna wa umeme na Nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati Mhandisi. Edward Ishengoma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba wakati akizindua mradi wa utekelezaji wa matumizi bora ya nishati unaotekelewa na Wizara ya nishati kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa [UNDP] na umoja wa ulaya [EU]

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhandisi Mramba amesema mradi huo utakapokalika utawanufaisha zaidi wananchi na watumiaji wengine wa Nishati kwani unalenga kupunguza matumizi ya Nishati na kuongeza Nishati hali itakayosaidia kuinua uchumi.

‘’ kwa mfano hapa nchini tuna matumizi ya juu kabisa ambayo hayajawahi kutokea yalitokea mwezi Novemba ambayo hatujawahi kuyafikia wakati wowote ambayo ni megawati 1307 hizi megawati zikitumika vizuri kwa matumizi mazuri wataalam wanasema unaokoa asilimia 20 ya megawati hizo ambayo ni megawati 261 na kuwepo megawati za ziada 261 ambazo ni uwekezaji mkubwa kwa maana hakuna chanzo chochote cha umeme nchini kwa nishati zote kinachoweza kufika hapo’’ alisema.

Alisema mradi huo ni muhimu kwa Taifa kwa sababu utaongeza nishati na kupunguza matumizi ya nishati nchini ambapo nishati ikitumika vizuri inawezekana kuongeza uchumi na umeme kuwafikia kirahisi na kutosha kwa wananchi.

Injinia Ishengoma amesema matumizi bora ya nishati ni chanzo kizuri cha nishati katika nishati ile ile unayoitumia na kwamba upo uwezekano wa wanaotumia nishati ya umeme mkubwa kutumika kwa nusu yake.

Naye Mtaalamu wa miradi katika shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP Abasi Kitogo alisema mradi huo unaogharimu kiasi cha sh. Bil 22.9 utasaidia nchi na dunia kufikia malengo ya kupata umeme jadidifu na nishati bora.

Amesema kufanikisha kwa malengo ya mradi utaweza kufikisha malengo endelevu ya nchi ambayo yanamuunganiko na malengo mengine ikiwemo ya kupungua kwa umaskini na masuala ya kijinsia.

Naye Meneja mradi ya nishati kutoka umoja wa Ulaya Mhandisi Francis Songela amesema wanaamini kuwa matokeo ya mradi huo yatasaidia kutanua aidi masualamaima ya kuhamasisha matumizi ya nishati kwa njia bora.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...