Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mahakama
ya hakimu mkazi Njombe imemuhukumu Fadhili Ngoho (25) mkazi wa Ulembwe
halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe kwenda jela kifungo
cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 8.
Mahakama
imebainisha kuwa kesi No 193/2020 ilikuwa ikimkabili mshtakiwa Fadhili
Ngoho ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka mtoto wa
miaka 8 ambaye ni mtu na mtoto wake wa kumlea/mtoto wa kambo aliyekuwa
akisoma katika moja ya shule ya msingi iliyopo katika kata ya Ulembwe
Inaelezwa kuwa siku hiyo mshtakiwa alimbaka mtoto huyo na kumwambia asipige kelele.
Mnamo
tarehe 23/2/2020 mama wa mtoto huyo alimuona mwanae hatembei vizuri
ndipo alipomuuliza ana tatizo gani na kisha binti huyo akamwambia mama
yake kuwa baba yake wa kambo alimbaka
Tarehe
24/2/2020 mama yake alikwenda kwa mtendaji wa kijiji kutoa taarifa juu
ya tukio hilo na alipewa barua ya kwenda polisi, mama huyo alifanya
hivyo na taratibu za kumpeleka hospitali mtoto ziliendelea.
Hukumu
hiyo imesomwa mbele ya Hakimu mfawidhi wa mkoa wa Njombe Liad Chamshana
huku ikiendeshwa na wakili wa serikali Andrew Mandwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...