Na Edwin Moshi, MAKETE.
Wanafunzi
wahitimu wa kidato cha 6 katika shule ya sekondari ya Wasichana Makete
(Makete Girl's) wametakiwa kutambua kuwa kila mmoja maisha yake
anayapanga kutoka kichwani kwake kwenda kwenye moyo wake na wasikubali
kidato cha sita kiwe ndio mwisho wao kielimu
Hali kadhalika
wametakiwa kuwaripoti wazazi ama walezi ambao wanawataka wahitimu hao
waolewe baada ya kuhitimu kwa kuwa ni kosa kisheria ili hatua
zichukuliwe
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Mstaafu
Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Kwanza ya
kidato cha 6 katika shule hiyo ambayo ilianzishwa wakati wa uongozi
wake na yeye akiwa miongoni mwa waliofanikisha uwepo wa shule hiyo
Matiro
amesema wanafunzi hao wanapaswa kuwa na malengo ya juu zaidi pamoja na
kufahamu kwamba kumaliza mitihani sio mwisho wa masomo bali ndio mwanzo
wa masomo kwani wanatarajiwa kuendelea na masomo katika vyuo vikuu ama
vyuo vingine mbalimbali hapa nchini
Amewasihi wanafunzi hao
kwenda kuitangaza vema shule hiyo huko wanakokwenda kwa kufanya vizuri
katika mitihani yao ya taifa pamoja na kuchukua mambo mazuri
waliyofundishwa na walimu wao na wakayaishi huko wanakokwenda
Pia
Matiro ameipongeza serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea kuiboresha shule hiyo kwani imeendelea kuboreshwa tofauti na
alivyoiacha wakati akiwa mkuu wa wilaya
Suala la shule hiyo
kukosa gari ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili shule hiyo kama
ilivyoelezwa kwenye taarifa fupi ya shule iliyosomwa na Mwl. Matinya,
Makamu Mkuu wa Shule hiyo kwa niaba ya Mkuu wa shule pamoja na risala ya
wahitimu kwa mgeni rasmi, ambapo imejibiwa na mgeni rasmi kwamba tayari
halmashauri inalishughulikia suala hilo na litatatulika muda si mrefu
Baadhi
ya wahitimu waliozungumza na mwandishi wetu akiwemo Marieta Yohana na
Anna David mbali na kuahidi kufanya vizuri kwenye mitihani yao ili
kuendelea kuitangaza vizuri shule yao, pia wanaimani changamoto
zinazoikabili shule hiyo zitaendelea kutatuliwa na serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...