Na Khadija Kalili

 Chama Cha Waajiri  nchini  
(ATE) kimeahidi kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na wadau wake ambao ni Mashirika binafsi, watu wenye ulemavu  pamoja na Serikali katika kusimamia  masuala ya ajira .

Akizungumza leo katika Ofisi za ATE zilizopo Mikocheni Dar Es Salaam Meneja  wa ATE Kanda ya Kati Dodoma Leonard  Selestini alisema  hayo katika mkutano uliowakutanisha  na Jumuia ya watu wenye Ulemavu  nchini ambao ni TASI,TLB na CHAVITA.

 Wakizungunza kwa nyakati tofauti watu  wenye ulemavu wamesema kuwa bado kunachangamoto nyingi katika utekelezwaji wa sheria ya kupata ajira.

Katibu wa Tanzania Albinism Society (TASI) Mussa Kabimba alisema kuwa "Tuko hapa kujadili sheria inayoihusu utekelezwaji wa upatikanaji wa ajira kwa watu wenye ulemavu nchini sababu bado kunachangamoto  nyingi ambazo watu wenye ulemavu wanakumbana nazo katika upatikanaji wa ajira hivyo tuko hapa kujadili ili nao waweze kunufaika" alisema Kabimba.

Katika  mkutano  huo watu hao wenye ulemavu waliweza  kutoa maoni  mbalimbali na kuishauri ATE iweze kuweka utaratibu wa kufanya ufuatiliaji kwa watu wenye ulemavu pindi wanapoajiriwa hii itasaidia kung'amua changamoto wanazokumbana nazo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...