Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
Ikumbukwe kwamba Serikali ilitangaza kurejesha Sh100 katika mafuta, pamoja na hayo bei hiyo ya nishati imeendelea kupanda.
Bei ya nishati ya Mafuta inapanda wakati wananchi wakilalamika kupaa kwa bei za bidhaa mbalimbali za vyakula hasa wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Aprili 5, 2022 Mkurugenzi wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Gerald Maganga amesema kuanzia kesho Jumatano, Aprili 6,2022 bei mpya ya petrol kwa mafuta yanayopokelewa kupitia Bandari ya Dar es salaam itakuwa Sh2,861 kutoka Sh 2,540 ikiwa ni ongezeko la Sh321.
Dizeli bei mpya itakuwa Sh2,692 kutoka Sh2,403 ya sasa ikiwa ni ongezeko la Sh289. Bei ya mafuta ya taa itapanda kutoka Sh2,208 hadi Sh2,682 ikiwa ni wastani wa Sh474.
Mafuta ambayo yatapitia Bandari ya Tanga, bei ya petrol itakuwa Sh2,848 kutoka Sh2,563 ikiwa ni ongezeko la Sh285.- Amesema Maganga
Upande wa dizeli bei itaongezeka kutoka Sh2,484 hadi Sh2,779 ikiwa ni ongezeko la Sh295 kwa lita moja.
Aidha mafuta ambayo yatapokewa kupitia Bandari ya Mtwara bei ya petrol kwa lita moja itakuwa Sh2,678 kutoka Sh2,577 ikiwa ni ongezeko la Sh100.
Bei ya dizeli kwa lita moja itakuwa Sh2,811 kutoka Sh2,530 ikiwa ongezeko la Sh281.
Hata hivyo, Maganga amesema kuwa bei hizo zimejumuisha tozo ya Sh100 ambayo Serikali ilitangaza kuiondoa mwezi Machi, 2022 kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kuirejesha akisema utaribu wa kuindoa haukufuatwa kwa kuwa fedha hiyo ilishapangiwa bajeti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...