KATIKA kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhan, Benki ya Exim Tanzania imefuturisha wateja wake visiwani Zanzibar.

Hafla ya futari hiyo ilifanyika Hotel Verde visiwani Zanzibar ikihudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wakiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Spika Zubeir aliishukuru benki hiyo kwa namna ilivyo karibu zaidi na wateja wake kwa kutambua na kuheshimu imani zao na hivyo kuamua kuonesha kwa vitendo heshima hiyo.

“Hatua hii inaleta faraja kubwa kiimani miongoni mwa wateja wenu na hivyo wateja wanajiona kuwa sehemu salama za si tu kibiashara bali kiimani…kwa hili nawapongeza sana Benki ya Exim,’’ alisema.

Akiwaasa waislamu katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Spika Zubeir alisema ni vyema walio na uwezo kuwafuturisha wasio na uwezo ili kujiongezea thawabu.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Ofisa Mkuu Idara ya Fedha Benki ya Exim, Bw Shani Kinswaga alisema benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhan kufuturu pamoja na wateja wake katika mikoa mbalimbali ili tu kuwatakia heri ya mfungo pamoja na kutoa shukrani kwa wateja wa benki hiyo na kuomba ushirikiano endelevu katika utoaji wa huduma za benki hiyo.

“Katika miaka yote ya utekelezaji wa shughuli zetu, Zanzibar imeendelea kuwa sehemu ya kimkakati kibiashara na tunaahidi kuendelea kushirikiana vema zaidi na wateja pamoja na Mamlaka mbalimbali za kiserikali na kidini katika kustawisha zaidi mahusiano yetu.’’

Katika kuthibitisha uhusiano wa kibiashara baina ya benki hiyo na wateja wake visiwani humo, Bw Kinswaga alisema tayari benki hiyo imekwisha toa mikopo mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya bil 30 kwa wateja wanaohudumu sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii.

“Pamoja na kufanya yote haya faraja kubwa kwetu imebaki kuwa ni ule mrejesho chanya tunaoupata kutoka kwa wateja wetu wanaotutambua kama benki yenye ubunifu na ubora. Hizi ni sifa ambazo tusingeweza kufikia bila uaminifu kutoka kwa wateja wetu…tunashukuru sana na tunaahidi kutowaangusha" alisema.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid akizungumza na wageni waalikwa waliohudhulia hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo iliyofanyika  Hotel Verde visiwani  humo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali.

Ofisa Mkuu Idara ya Fedha Benki ya Exim, Bw Shani Kinswaga  akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ya uongozi wa benki hiyo kwa wageni waliohudhulia hafla ya futari iliyoandaliwa na benki kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo iliyofanyika  Hotel Verde visiwani  humo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wakiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid.


Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim Bw Andrew Lyimo akizungumza  na wageni waliohudhulia hafla ya futari iliyoandaliwa na benki kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo iliyofanyika  Hotel Verde visiwani  humo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wakiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid



Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Zanzibar Bw Mwinyimkuu Ngalima akizungumza  na wageni waliohudhulia hafla ya futari iliyoandaliwa na benki kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo iliyofanyika  Hotel Verde visiwani  humo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wakiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid




Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhulia hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo iliyofanyika  Hotel Verde visiwani  humo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wakiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid (wa pili kushoto), akiwa ameongozana  na wageni wengine kupata futari wakati hafla ya futari iliyoadaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wake Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika Hotel Verde , Zanzibar ilihudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, viongozi wa chama, wateja, pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakati hafla ya futari iliyoadaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wake Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika Hotel Verde , Zanzibar ilihudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, viongozi wa chama, wateja, pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...