WAKATI nchi ya Tanzania ikipambana kuendelea kukua Kisayansi na Teknolojia, Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini COSTECH imeendelea kuwa elimu ya kutumia soko mtandao wabunifu kutoka kwenye Kongano 15 nchini.
Akizungumza kwenye warsha hiyo ya siku mbili jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Ubunifu na Teknoloji wa tume hiyo Dk. Gerald Kafuku, amesema kuwa Kongoni hizo zilizo chini ya mwamvuli wa COSTECH zimepewa mafunzo ya kuuza bidhaa zao walizobuni mtandaoni.
“Tumekutana na wafanyabiashara wadogo wabunifu, tunawaapa msaada wa teknolojia, wataalamu, kupitia vyuo vikuu na taasisi za utafiti “
Tumewapa mitambo pamoja na mitaji na leo tunawafndisha namna ya kuuza bidhaa zao za ubunifu ili ziwafikie watu wengi kirahisi” amesema Dkt. Kafuku.
Dkt Kafuku amesema jukumu la Tume hiyo ni pamoja na kuwasimamia wabunifu na kuwasaidia ili vijana wajiajiri na taifa kupata maendeleo.
Amesema kuwa COSTECH hadi kufikia mwezi wa saba itaongoza wabunifu wa sekta mbalimbali ikiwemo Madini, Mawese, na Korosho.
Naye Fatma Mohammed Omari Mwakilishi kutoka kongoni ya Pemba inayojishughulisha na usindikaji samaki kwa njia ya asilia na ile njia ya kuoka kwa moshi ameishukuru COSTECH kwa kuendelea kuwasapoti kwa kuwapa elimu ya kunadi bidhaa zao kwa njia ya mtandao.
“Tumepewa elimu juu ya kufanya biashara zetu kwa njia rahisi itakayowafikia wateja wengi kwa haraka bila gharama kubwa nayo ni njia ya mtandoa “ amesema Fatma.
Fatma amesema kuwa Dagaa za Zanzibar zimekuwa na soko huku nchini Kongo ambapo matamanio yake siku moja walifikie soko hilo bila madalali.
Kwa upande wake, Juma Mene Mwakili wa Kongoni ya Sindida inayojishughulisha na utengenezaji mafuta ya Alizeti, Sabani Mashudu ya Alizeti amesema kuwa Kongozi yao inauwezo wa kuzalisha Lita alfu 2 kwa siku ambapo kwa mafunzo hayo wataweza kupata wateja wengi zaidi.
Mene amesema kuwa endapo serikali itaweka mkazo kwenye zao hilo nchini itaachana na kuagiza mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...