NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO. 
CARE International Tanzania kupitia miradi yake ya TAJIRIKA NA KILIMO {TnK} na UJANA NI UCHUMI IMARA (UCHUMI) imetoa mafunzo kwa  wanawake na vijana elfu mbili na miambili ishirini (2,220) ili waweze kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo na ufugaji. 
Mradi wa TAJIRIKA NA KILIMO (TnK) na UJANA NI UCHUMI IMARA (UCHUMI) umetekelezwa na CARE International Tanzania kwa ubia wa VETA na SAGCOT center Ltd. imekuwa na mnaufaa makubwa kwa wananchi hususani wale walioko katika vikundi  vya kuweka na kukopa ambapo kundi kubwa la wanufaika hao ni wanawake na vijana. 
Akizungumza kwenye kikao kazi cha tathimini  ya miradi hiyo Mkurugenzi Mkazi wa CARE International Bi.Prudence Masako alisema  CARE wanalenga kuwafikia watu milioni miambili lengo likiwa ni kupunguza umasikini  kwa watanzania na kuleta haki hadi kufikia mwaka 2030 
Alisema CARE imekuwa ikifanya kazi kubwa katika kuangalia namna gani  jamii inaweza  kutumia rasilimali zilizopo  ili kujikwamua kiuchumi hususani kwa wanawake ambao wengi wao wamekuwa wakishindwa kujitetea na kukosa haki zao za msingi . 
Kwa upande wake Meneja msimamizi wa miradi kutoka CARE Bwana.Samwel Chambi alisema kuwa miradi hiyo ya TAJIRIKA NA UCHUMI imekuwa ikihamasisha  watu kujiunga katika vikundi na kujengewa uwezo hususani katika kilimo  biashara na uchumi hasa kwa wanawake na vijana . 
Aidha Chambi alibainisha kuwa mradi wa TAJIRIKA NA UCHUMI  imekuwa fursa kwani imewapatia  wanawake zaidi ya 3000 mafunzo ya ujuzi  na vijana 15,000 mafunzo ya ujasiriamali , stadi za maisha , jinsia na usawa. 
Hata hivyo imeelezwa kuwa fursa hizi zimetumika vyema kuchangia kupunguza tatizo la umasikini kwa vijana kwakuwa walengwa wamewezeshwa kuanzisha kilimo biashara na wengine ufugaji  ili kujikwamua kiuchumni. 
Akifungua kikao kazi hicho Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tixon Nzunda  ameviagiza vyuo vya ufundi stadi nchini VETA  kuanza kutekeleza mara moja  miataala ya   kilimo biashara na uchumi , ambayo tayari imekamilika  lengo likiwa ni kuongeza  ujasiliamali , kipato na kuimarisha uchumi wa wananchi   na Taifa kwa ujumla. 
Alisema taasisi zote zinazotoa mafunzo zihakikishe  zinatoa elimu ya mifugo na kilimo biashara ili vijana waweze kupata ujuzi na maarifa ya kilimo na ufugaji bora. 
Hata hivyo alizitaka taasisi za mafunzo ikiwemo VETA, MATI NA LITA na sekta binafsi kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anatoa ushirikiano wa kutosha ili matokeo ya kazi zilizofanyika na miradi ya kilimo  na uchumi  zinaendelea kuwanufaisha wanajamii hata wale ambao hawakufikiwa moja kwa moja na miradi ya Tnk na UCHUMI.
 Kikao hicho kilichofanyika mkoani Morogoro kimehudhuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo na mifugo, wakurugenzi  na wataalamu wa kilimo na mifugo kutoka Halmashauri zote ambazo miradi imetekelezwa pamoja na wanufaika wa miradi hiyo
Mkurugenzi
 Mkazi wa CARE International Bi.Prudence Masako akizungumza kwenye kikao
 kazi cha tathimini  ya miradi TAJIRIKA NA KILIMO (TnK) na UJANA NI 
UCHUMI IMARA (UCHUMI) kilichofanyika April 22, 2022Mjini Morogoro. 
Baadhi ya wadau wa kilimo na mifugo walioshiriki katika kikao hicho. 
Katibu
 Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tixon Nzunda akizungumza kwenye kikao 
kazi cha tathimini  ya miradi TAJIRIKA NA KILIMO (TnK) na UJANA NI 
UCHUMI IMARA (UCHUMI) kilichofanyika April 22, 2022Mjini Morogoro. 
   


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...