Na Jane Edward, Arusha
Zaidi ya Bilioni mbili za Kitanzania zilizotolewa na shirika la Kimataifa la maendeleo Duniani (CBM)lenye makao yake makuu nchini Ujerumani zinatajwa kutumika Katika ujenzi wa hospitali kubwa na ya kisasa Mkoani Mwanza katika hospitali ya Bugando,ambapo ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 95.
Hayo yameelezwa jijini Arusha na Nesia Mahenge Mkurugenzi Mkazi CBM Tanzania katika Mkutano mkubwa wa kimataifa uliowashirikisha wataalamu mbalimbali kutoka nchi za nje ikiwemo UK,Paragway,nchi za kiafrika ambapo mwenyeji wa Mkutano huo ni CBM Tanzania.
Amesema kuwa ujenzi huo lengo lake ni kuhakikisha walemavu wa macho ,masikio pamoja na mambo mengine wanapata huduma zote kwa urahisi katika hospitali zote ikiwemo KCMC ambayo wanashirikiana nayo kwa ukamilifu.
Aidha amesema kwa sasa wanaendelea kutoa mafunzo kwa madaktari ili waweze kutoa huduma inayotakiwa kwa viwango vya Kimataifa kwa kushirikiana na hospitali ya Bugando, na CBM imejipanga kuhakikisha kwa Tanzania wanapunguza kabisa matatizo ya macho.
Ameongeze kuwa CBM wamezindua mradi wa kuangalia dalili za awali kwa mgonjwa kwa kutumia simu ya kiganjani ili kujua matatizo ya macho kwenye jamii ambapo huduma hiyo ipo pia Wilayani Hai na Mwanga Mkoani Kilimanjaro ambapo lengo ni kutoa huduma zote za macho ili ziweze kutumia teknolojia katika zoezi la upimaji.
Amefafanua kuwa mpango ambao upo kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mwananchi anapimwa vipimo vya awali ili kugundua kama ana tatizo na kulipatia ufumbuzi ambapo tayari baadhi ya wataalamu wamepatiwa simu hizo.
"Kwa Kanda ya kaskazini tayari kuna mdau ambaye ni KCMC ambapo wanaangalia Mkoa moja wapo wa kuweka hospitali ili kusaidia wananchi wa kanda hii kutotembea umbali mrefu kufuata huduma"Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Afrika mashariki na Afrika ya kusini CBM Albert Kombo, anasema kuwa wamepata usaidizi mkubwa kutoka kwa serikali ya Tanzania na kwamba wanaangalia ni teknolojia gani inaweza kutumika katika kutatua changamoto za uoni.
Anasema wamekutana kwa wiki nzima jijini Arusha ili kujadiliana na kuona ni namna gani wanaweza kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi na namna sahihi ya kuzitoa.
"Kila mmoja anatakiwa kujiuliza ni kuwa ukiwa kipofu itakuwaje na kwamba itapunguza nguvu kazi ya familia na hautaweza kuhudumia watu wako wala jamii kwa ujumla na kwamba wanaangalia asilimia themanini ya watu kutokuwa vipofu"kasilimia Alisema
Amebainisha kuwa wanaishukuru serikali ya Tanzania kwa namna wanavyotoa ushirikiano kwa shirika hilo katika kuhakikisha Tanzania inapunguza changamoto ya uoni kwa asilimia kubwa.
Nesia Mahenge akiwa na Dr Babar Quresh Mkurugenzi wa Kimataifa wa afya na macho na Makamo wa Rais wa IAPB.
Nesia mahenge Mkurugenzi Mkazi CBM Tanzania Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...