Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimesikia na kuona kupitia vyombo vya habari kuwepo
kwa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambao wamedai kuwa
wanawakilisha kampuni saba wakilalamika kuidai fedha Kampuni ya Uhuru
Media Group (UMG) kutokana na kandarasi za kuzalisha huduma mbalimbali
kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Kupitia kauli zao zilizonukuliwa katika baadhi ya vyombo vya habari siku ya Jumatano Aprili 27, mwaka huu watoa huduma hao wamedai kuwa jumla ya kampuni 7 wanazoziwakilisha zinaidai kampuni hiyo ya UMG jumla ya Shilingi bilioni moja yakiwa ni malipo na malimbikizo ya madai yao baada ya kutoa huduma za kutengeneza na kusambaza sare na mabango wakati wa kampeni hizo.
Kupitia taarifa hii, Chama Cha Mapinduzi kinatoa kauli kuwa, kinatambua kuwepo kwa madai yakiwemo madeni ya fedha kwa Kampuni ya UMG kutokana na shughuli mbalimbali za kibiashara inayofanya. Kutokana na kutambua hilo, tayari Chama kimeshachukua hatua mbalimbali zikiwemo zinazoendelea sasa za kufanya uhakiki ili kujiridhisha uhalali wake, kabla ya kuendelea na mchakato mwingine baada ya kujiridhisha.
Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu CCM Taifa,
Itikadi na Uenezi
28 Aprili 2022.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...