Baadhi ya wananchi wakiwa tayari katika Viwanja vya AICC wakisubiria uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour
Baadhi ya wananchi wakiwa tayari katika Viwanja vya AICC wakiwemo Viongozi wa dini mbalimbali wakisubiria uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour

Wadau mbalimbali wa Utalii wakiwa Baadhi ya wananchi wakiwa tayari katika Viwanja vya AICC wakisubiria uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour
Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda Akiwa na vijana wa bodaboda katika Viwanja vya AICC ambapo aliwaongoza katika kuhakikisha wanashuhudia uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour

Baadhi ya wananchi wakiwa tayari katika Viwanja vya AICC wakisubiria uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour

Burudani ikiendelea katika Viwanja vya AICC wakisubiria uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour


Na.Vero Ignatus,Arusha


Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda ameongoza vijana zaidi ya mia moja waliotoka kumpokea mh Rais Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro na lengo kubwa ni kuunga mkono juhudi za mh rais katika uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour.

Akizungumza na Michuzi Blog Mtanda amesema kuwa Sasa hivi wanahamasika kuhamasisha wawekezaji,hoteli na wafanyabaishara wa kati na wakubwa na wapo katika mazungumzo na pamoja na mabeki ili waweze kuwekeza

Kwa upande wake mdau wa Utalii Amosi Nko kutoka TTB wamemshukuru Rais kwa kazi kubwa na ubunifu wake amesema wanategemea kuwa utalii utaongezeka na kuongeza kipato kutokana na mazao ya utalii

Nko amesema kuwa mwaka 2025 mapato ya utalii yanatakiwa kuongezeka hadi kufikia bil 6 hivyo kw akupitia Royal Tour
Itakuwa utambulishi wa nchi na kuvutia wawekezaji mbalimbali katika kuboresha maeneo mabalimbali ya utalii.

Akizungumza mmoja wa wananchi ambae ni mfanyabiashara katika jiji la Arusha Digner Nassary amesema kuwa uzinduzi huo unao manufaa makubwa kwao kwani kioato Chao kitaongezeka kutokana na wageni kuja kununua bidhaa mbalimbali wanapotembekea vivutio vya vilivyopo

"Unajua uzinduzi huu wa hii filamu ni faida Sana kwetu,tofauti na awali kutokana na Ile changamoto ya Covid 19 aisee mambo hayakuwa mazuri hata kidogo maana tulikuwa ahatuuzi maana wageni walikuwa hawaji nchini"alisema Digner

Aidha Kwa upande wa wananchi walianza kuingia katika Viwanja vya Kituo Cha mikutano Cha Kimataifa Cha AICC kuanzia saa moja asubuhi kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour
Naye Erasto Kisanya,alisema uzinduzi wa filamu hiyo utasaidia kwa kasi kutangaza vivutio vya kitalii vilivyopo nchini.

"Mimi kama mwananchi wa kawaida sikuwahi kutegemea kama Rais atatengeneza filamu kama hii ambayo itaitikisa dunia,haswa katika eneo la vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania,"anasema Nabulu Laizer

"Hivyo tunayo haja ya kuiga mfano huu wa kishujaa ambao Rais ameuonyesha kwetu na tumuunge mkono katika kutangaza vivutio hivi,ambapo kupitia filamu hii tutaitangaza nchi yetu kwa haraka zaidi"anasema Nabulu Laizer

Aidha katika kushiriki katika shamrashamra za uzinduzi wa Royal Tour zaidi ya vijana 100 vijana 100 waliandamana kumpokea mhe.Rais katika kiwanja Cha Ndege KIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...