Na. Damian Kunambi, Njombe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Mpango amewataka vijana 6 waliopewa dhamana ya kukimbiza mwenge kwa mwaka huu 2022 kuhakikisha kuwa wanakagua miradi kwa usahihi na kujiridhisha juu ya thamani za fedha zilizotumika zinaendana na miradi hiyo.
Maagizo hayo ameyatoa wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge uliofanyika katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe ambapo mbio hizo zitaongozwa na mmoja wa vijana hao kutoka mkoa wa Njombe Sahili Nyanzabara Geraruma.
Amesema kuwa vijana hao wanapaswa kuifanya kazi hiyo ipasavyo bila woga wowote na na endapo watabaini utofauti wa matumizi ya fedha hizo za miradi wahakikishe wanatoa taarifa katika vyombo husika.
Sanjari na hilo pia amewataka Viongozi wote Nchini kuenzi falsafa za waasisi wa Taifa hili ikiwemo kuanzishwa Kwa Mwenge wa Uhuru ambao ulikuwa na lengo la kuleta matumaini kwa Watanzania pamoja na Kukemea Vitendo vya Rushwa,Dhuluma na Ufisadi.
" kwa kuzingatia falsafa za viongozi waasisi wa Taifa hili ni wajibu wa kila kiongozi kutekeleza Kwa vitendo upingaji wa rushwa, dhuluma pamoja na Ufisadi"
Mwenge huu wa Uhuru utakimbizwa kwa siku 195 katika Halmashauri za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na katika mikoa 31 na kisha kuhitimishwa tarehe 14 0ctober 2022 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani.
Home
HABARI
DKT. MPANGO AWATAKA VIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KUTOOGOPA KUIKATAA MIRADI ISIYOKIDHI VIGEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...