Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutumia mkaa mbadala (Rafiki Briquettes) utokanao na madini ya makaa ya mawe ili kuchangia utunzaji wa uoto wa asili na kupunguza uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji miti.
Elimu hii imetolewa kupitia maonesho yaliyoandaliwa wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika Aprili 1, 2022 katika viwanja vilivyopo Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini DODOMA.
Akiongea kuhusu mpango mkakati wa STAMICO katika kuutangaza mkaa huo Bw. David Semeo amesema Shirika limejidhatiti kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kufikisha elimu kuhusu Mkaa huu kwa watu mbalimbali.
Amesema mkaa huu umeletwa ili kuleta tija kwa mazingira ya nchi yetu na utumiaji wa mkaa huu utapunguza kasi ya ukataji miti katika maeneo mengi ya nchi hivyo mkaa huu ni rafiki kwa mazingira, matumizi.
Akiongea wakati alipotembelea banda la STAMICO Bw. Sixtus Mapunda mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi amesema mkaa huu utaleta tija kwa wananchi endapo utawafikia hadi wananchi wa vijijini.
"Mkaa huu unaonesha kuleta tija sana kwa wananchi wote hasa wanaotumia nishati ya mkaa wa miti, hivyo ni vyema Shirikia likajipanga kuzalisha kwa wingi na kuusambaza kwa wananchi"
Naye Dkt. Brighton Gwamagobe ameipongeza STAMICO na kusema kuwa inatakiwa kuhakikisha inapata vyeti vya udhibitisho wa kutokuwepo kwa sumu mbalimbali ili mkaa huo uweze kutumika kimataifa.
Shirika linaendelea kutoa elimu ya mkaa wa Rafiki Briquette kupitia mikutano, makongamano mbalimbali ili kuchochea matumizi ya mkaa huo ambao umetengenezwa kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani, mashuleni na maeneo mengine yenye uhitaji wa nishati ya kupikia kama hii.
Mhandisi Migodi wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Haruni Mbaraka( kulia) akimhudumia mwananchi katika mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jijini Dodoma,
Mmoja wa wananchama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika banda la STAMICO wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...