Na.Khadija Seif, Michuzi TV
SHINDANO kubwa la kihistoria la Mchezo wa Gofu "European Tour Challenge" ambalo limeahirishwa Kwa mwaka huu,ambapo lilitarajiwa kufanyika mapema April 7 mwaka huu Mkoani Arusha.
Akizungumza Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania( TGU ) Chris Martin ameomba radhi kutokana na usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na kughairishwa kwa Shindano hilo na amewataka wachezaji na wadau wa Mchezo huo wajiandae kwa ajili ya shindano hilo litakalofanyika mwakani.
European Tour Challenge lilitarajiwa kufanyika April 7 hadi 10 mwaka huu katika Klabu ya Gofu ya Kill Gofu jijini Arusha lakini kutokana na sababu zilizojitokeza shindano hilo litafanyika Febuari 2023.
Shindano hilo ambalo awali liliotarajiwa kuhudhuriwa Kwa Klabu mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi chama kilijikita zaidi kuhakikisha Mchezo huo wa gofu unakua na sehemu ya kutangaza utalii wa ndani Ili kuunga Mkono juhudi za mama Samia.
Mwenyekiti wa Chama cha Gofu nchini (TGU) Chris Martin akitolea ufafanuzi kuhusiana na kuahirishwa kwa Shindano la "European tour challenge" lililotarajiwa kufanyika mapema April 7 mwaka huu katika Klabu ya kill gofu Mkoani Arusha Kwa Sasa wanajipanga na Shindano hilo kufanyika mwakani mwezi February
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...