Na.Khadija Seif, Michuzi TV

TAASISI ya Kusaidia watu wenye uhitaji (Happy Hands) wameukaribisha Mwezi mtukufu wa Ramadhani Kwa kugawa Mahitaji mbalimbali ya vyakula jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Michuzi TV Mmoja ya Mwakilishi kutoka taasi hiyo Zainab Ally amesema mara Kwa mara wamekuwa wakiukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani Kwa kuwagawia Mahitaji mbalimbali kwa makundi yenye uhitaji .

Zainab amesema kufunga Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni Moja ya amrisho ambalo Kila Muumin wa kislaam ambae Hana tatizo lolote la Kiafya anawajibika kutimiza funga zake.

Hata hivyo amewatakia heri waumini wote wa dini ya kiisilam katika kupokea Mwezi huo na kuwakumbusha kumaliza salama na kuwa watulivu na Mahitaji hayo ambayo wamepatiwa Kwa baadhi ya watu kutumia na wasiojiweza.

Baadhi ya vyakula ikiwemo Mchele,Sukari ,Mafuta ya kupikia,Unga,Maharage na tambi vikiwa ndani ya vikapu tayari Kwa kugawiwa Kwa watu wenye uhitaji wa dini ya kiisilam ikiwa ni sehemu ya kuukaribisha Mwezi mtukufu wa Ramadhani
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...